Ijumaa, 29 Mei 2026

JAJI MFAWIDHI IRINGA AFANYA UKAGUZI WA MAHAKAMA ZA MWANZO

·        Asisitiza kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na uwajibikaji

·        Apongeza wananchi kusaidia kukarabati jengo la Mahakama

Na LUSAKO MWANG’ONDA, Mahakama- Iringa

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Iringa, Mhe. Dunstan Ndunguru amefanya ziara ya ukaguzi wa Mahakama za Mwanzo katika Wilaya ya Iringa ambazo ni Mlolo, Ifunda na Kiponzero na kuwataka watumishi wa Mahakama hizo kufanya kazi kwa Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji.

Katika ziara hiyo iliyofanyika hivi karibuni, Mhe. Ndunguru alipokea taarifa za utendaji kazi wa Mahakama hizo za Mwanzo, zilizofafanua baadhi ya mafanikio na changamoto katika utendaji kazi mathalani uchakavu wa majengo ya Mahakama, upungufu wa watumishi na sehemu ya majengo ya kutolea huduma kukosa umeme.

Mhe. Ndunguru aliwapongeza watumishi wa Mahakama hizo kwa jitihada wanazozifanya katika kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani na pia utekelezaji wa Mpango Mkakati waliojiwekea wa kupunguza Mahabusu gerezani na kuwezesha idadi ya mahabusu kupungua kwenye Magereza yaliyo katika Mkoa wa Iringa.

Vilevile, Jaji Ndunguru aliwasisitiza Mahakimu wa Mahakama hizo kushughulikia mashauri ya mirathi kwa weledi na uadilifu na pia kuhakikisha wanufaika wa mirathi hiyo wanalipwa stahiki zao kwa wakati na kuwahimiza wanufaika hao kufunga mashauri hayo baada ya kukamilika kwa taratibu husika.

“Moja ya vipaumbele vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Iringa ni kuhakikisha wanufaika wa mirathi wanalipwa na kwamba wasipolipwa kwa wakati inaleta taswira kwamba Mahakama ina miliki fedha nyingi ambazo kimsingi ni za warithi wa marehemu,” alieleza Jaji Mfawidhi huyo.

Akizungumza katika vikao alivyofanya na watumishi wa Mahakama hizo, Mhe. Ndunguru aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na upendo hasa wakiongozwa na salamu ya Mahakama ambayo ni nguzo ya utendaji kazi mahakamani ya, ‘Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji’ ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi katika utoaji haki.

Aidha, Mhe. Ndunguru alitumia ziara hiyo kukutana na kuushukuru Uongozi wa Kata ya Kiponzelo kwa jitihada zao za kuisaidia nguvu kazi Mahakama katika kukarabati jengo la Mahakama ya Mwanzo ya Kiponzelo na kuwezesha kuanza kwa shughuli za Mahakama ambazo kwa kipindi kirefu zilikuwa zimesimama kutokana na uchakavu wa jengo hilo.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Iringa, Mhe. Dustan B. Ndunguru akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Mahakama ya Mwanzo Mlolo kwa ajili ya kufanya ukaguzi hivi karibuni.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Iringa, Mhe. Dustan B. Ndunguru (kushoto) akipokelewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Mlolo alipotembelea hivi karibuni kwa ajili ya ukaguzi.
     
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Iringa, Mhe. Dustan Ndunguru akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Mahakama ya Mwanzo ya Ifunda kwa ajili ya kufanya ukaguzi.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa Mhe. Dustan Ndunguru akiagana na baadhi ya Viongozi wa Kata ya Kiponzelo baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Kiponzelo.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

 

Maoni 1 :

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta