Jumanne, 12 Mei 2026

MTENDAJI MKUU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA TUGHE WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 12 Mei, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wa Mahakama ya Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick pamoja na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mahakama ya Tanzania, Bi. Alice Haule.

Lengo la kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka kabla ya Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ni kujadili pamoja kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu watumishi wa Mahakama sambamba na kujadili hoja za Mabaraza ya Kanda na Divisheni za Mahakama Kuu kwa upana zaidi kabla ya kufanyika kwa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania.

Aidha, Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania kinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Mei, 2026 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju.

Yafuatayo ni matukio katika picha ya Kikao kati ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wa Mahakama ya Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wa Mahakama ya Tanzania leo tarehe 12 Mei, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wa Mahakama ya Tanzania (hawapo katika picha) leo tarehe 12 Mei, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Aliyeketi kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mahakama ya Tanzania, Bi. Alice Haule.


Picha mbalimbali za Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha) alipokuwa akizungumza nao leo tarehe 12 Mei, 2026 Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick akiwa katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mahakama ya Tanzania, Bi. Alice Haule akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.


Viongozi mbalimbali wa TUGHE Mahakama wakichangia juu ya masuala mbalimbali ya Watumishi wa Mhimili huo wakati wa Kikao na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kilichofanyika leo tarehe 12 Mei, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.

Meza kuu ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ikisikiliza na kurekodi hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa TUGHE-Mahakama ya Tanzania leo tarehe 12 Mei, 2026 jijini Dodoma.


Meza kuu ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiandika hoja na michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na Viongozi wa TUGHE-Mahakama ya Tanzania wakati wa kikao.

(Picha na MARY GWERA & ARAFA RUSHEKE, Mahakama-Dodoma)








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni