Jumatano, 20 Mei 2026

RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI TISA WAPYA WA MAHAKAMA YA RUFANI

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Majaji tisa wa Mahakama Kuu kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Bakari Machumu, leo tarehe 20 Mei, 2026, imesema kuwa wateule hao wataapishwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Walioteuliwa ni Majaji saba wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wawili kutoka Mahkama Kuu ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Abdi Shaaban Kagomba na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Arusha, Mhe. Yohane Bokobora Masara.

Wengine ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi na Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Rabia Hussein Mohamed.

Wateule wengine ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam, Mhe. Cyprian Phocas Mkeha na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina.

Wengine ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, Mhe. Iman, Daud Aboud, Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Laurent Masabo.


Mhe. Abdi Shaaban Kagomba.

Mhe. Yohane Bokobora Masara.

Mhe. Immaculata Kajetan Banzi.

Mhe. Rabia Hussein Mohamed.

Mhe. Cyprian Phocas Mkeha.

Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina.

Mhe. Iman, Daud Aboud.

Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim.


Mhe. Dkt. Juliana Laurent Masabo.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni