Marehemu Iddi Nassibu Chumu enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Iddi Nassibu Chumu aliyekuwa akifanya kazi Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kama Ofisa Usafirishaji (Dereva).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Mei, 2026 na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick marehemu Iddi amefikwa na umauti leo Jumamosi tarehe 23 Mei, 2026 Saa 7 Mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Bi. Beatrice amesema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea. Marehemu Iddi anatarajiwa kuzikwa Siku ya Jumapili tarehe 24 Mei, 2026 Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu Iddi Nassibu Chumu.
HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE YEYE TUTAREJEA (INNA LILLAH WA INNA ILLAH RAJIUN).



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni