Jumanne, 26 Mei 2026

TMJA SONGEA YAFANYA MKUTANO WA ROBO YA KWANZA 2026

Na NOEL SYLIVESTER-Mahakama, Songea

Chama cha Mahakimu na Majaji Songea tarehe 22 Mei 2026 kilifanya mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka 2026, ikiwa ni kutekeleza matakwa ya Katiba yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria.

Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Heritage Cortage (Padogo Pazuri) ulioko Msamala Songea Mjini ulifunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Songea, Mhe. James Karayemaha, ambaye ndiye mlezi wa chama hicho kwenye Mkoa wa Ruvuma.

Mkutano huo ulio hudhuliwa na Wanachama 58 kutoka Mahakama Kuu Songea (5), Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea (2), Mahakama ya Wilaya Songea (15), Mahakama ya Wilaya Mbinga (11), Mahakama ya Wilaya Namtumbo (10), Mahakama ya Wilaya Tunduru (10) na Mahakama ya Wilaya Nyasa (5).

Katika mkutano huo, Wanachama walijadili malengo ya TMJA Songea, ikiwemo kukuza uhuru wa Mahakama kama msingi wa kulinda haki za binadamu na uhuru, kukuza haki, maslahi na ustawi wa wanachama.

Malengo mengine ni kukuza na kulinda heshima ya ofisi ya Mahakimu na Majaji, kuongeza au kuimarisha ujuzi na uelewa wa Mahakimu na Majaji katika majukumu yao kwa kuendeleza tafiti na elimu (kuwajengea uwezo) na kutoa tuzo kwa Wilaya itakayofanya vizuri ili kuenzi kazi zao.

Katika mkutano huo, Katibu wa TMJA Songea, Mhe. Shughuli Mwapashe, alisoma tarifa fupi ya chama na kugusia vipengele mbalimbali kama mahusiano ya TMJA na Mwajili, mafunzo na semina kwa Wanachama, mafanikio pamoja na changamoto.

“Mafanikio ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliobora kati ta TMJA na Mwajiri, kutoa elimu kwa umma kila jumatano katika kituo cha redio (selous fm) na kwenye viunga vya Mahakama, kabla ya kuanza kusikiliza mashauri na uanzishwaji wa kamati ya kuandaa majarida na elimu.

Alieleza changamoto zilizopo katika chama kama vile baadhi ya Wanachama kukosa hamasa ya chama pamoja na ufinyu wa bajeti, jambo ambalo limekuwa likisababisha Tawi kishindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa wakati.

Katibu huyo aliahidi kutimizaa kwa vitendo vigezo maalum vya kupima utendaji na ubora wa mfumo wa Mahakama kama ilivyoelekezwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, katika hotuba yake ya tarehe 13 Januari, 2026 wakati wa kufungua mkutano mkuu wa TMJA jijini Dodoma.

Vigezo hivyo ni uadilifu, uwezo wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi, kuwiwa kuona haki inatendeka, ubunifu, uchukuaji wa hatua mapema, uzalendo na kuzingatia uhalisia wanapotekeleza majukumu yao.

Mgeni maalum katika mkutano huo, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bi. Marry Makondo, katika hotuba yake aliwapongeza Mahakamu na Majaji kwa kusaidia kwenye upatikanaji wa haki kwa wakati.

Katika hotuba yake, Mhe. Karayemaha aliwasisitiza wanachama kujitoa katika kushiriki matukio yanayohusiana na chama na kushirikiana kwa hali na mali.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Songea, Mhe. James Karayemaha wakati wa kufungua mkutano wa TMJA Tawi la Songea.

Jaji wa Mahakama Kuu Songea, Mhe. Emmanuel Kawishe. (aliye simama).

Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bi. Marry Makondo, akitoa hotuba kwa Wanachama wa TMJA Tawi la Songea.

Mwenyeki wa TMJA Tawi la Songea, Mhe. Saada tagalile,  wakati akitambulisha meza kuu.

Katibu wa TMJA Tawi la Songea, Mhe. Shughuli Mwampashe.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama Kuu Songea (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Wilaya Songea (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Wilaya Mbinga (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Wilaya Nyasa (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Wilaya Namtumbo (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Wanachama wa TMJA kutoka Mahakama ya Wilaya Tunduru (waliosimama) kwenye picha ya pamoja na meza kuu.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni