Jumatatu, 8 Juni 2026

DCM YAFANYA TATHIMINI YA MWENENDO WA MAHAKAMA INAYOTEMBEA MBEYA

Na. MUKSINI NAKUVAMBA - Mahakama, Mbeya

Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) ilifanya ziara katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya hivi karibuni kutathimini juu ya hali ya utoaji wa huduma zitolewazo na Mahakama Inayotembea katika Masjala hiyo.

Katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Mahakama Kuu Masjala hiyo kikiongozwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) Mhe. Moses Betwel Ndelwa, ili kujadili juu ya changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utoaji wa huduma za Mahakama Inayotembea.

 Aidha, Mhe. Ndelwa aliwasisitiza wasimamizi na watumiaji wote wa gari la Mahakama Inayotembea (Mobile court Service) kuzingatia misingi na taratibu za matumizi ya gari hilo.

“Matumizi ya Gari la Mahakama Inayotembea (Mobile court Service) yazingatie huduma za Mahakama Inayotembea tu na si vinginevyo,” alisisitiza Mhe. Ndelwa

Mhe. Ndelwa aliongeza kuwa, usikilizwaji wa mashauri kwenye Mahakama Inayotembea usizidi siku thelathini (30) tangu tarehe ya kufunguliwa kwa shauri. Sambamaba na hilo aliwasisitiza watumishi wanaofanya kazi katika Mahakama Inayotembea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu na kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma bora za kimahakama.

Vilevile, Mhe. Ndelwa aliwashukuru Idara ya fundi sanifu, umeme, maji na TEHAMA Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye Gari la Mahakama Inayotembea na kupelekea utendaji bora wa kazi. 

Pia aliwaasa Mahakimu Wafawidhi Mkoa na Wilaya ya Mbeya kufanya ziara za mara kwa mara ili kufuatilia hali ya huduma zitolewazo kwenye Mahakama inayotembea.

Sambamba na kikao hicho, ugeni huo ulifanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya Gari linalotoa huduma ya Mahakama inayotembea na kutembelea moja ya kituo cha kutolea huduma za Mahakama inayotembea katika Kata ya Uyole ndani ya jiji la Mbeya na kujionea Mazingira ya utolewaji wa huduma za Mahakama Inayotembea kwa  wananchi.

Mwenyekiti wa kikao, Naibu Msajili Mahakama ya Tanzania kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) Mhe. Moses Betwel Ndelwa (katikati) akizungumza katika kikao cha Tathmini ya utendaji kazi wa Mahakama Inayotembea, kulia ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu na kushoto ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhe. Sifa Jacob.

Maafisa Mahakama kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) wakiwa katika ziara ya kutembelea moja ya kituo cha kutolea huduma ya Mahakama inayotembea (Mobile Court Service) 

Maafisa Mahakama kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) wakiwa katika ziara ya kutembelea moja ya kituo cha kutolea huduma ya Mahakama inayotembea (Mobile Court Service) 


Maafisa Mahakama kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) wakiwa katika ziara ya kutembelea moja ya kituo cha kutolea huduma ya Mahakama inayotembea (Mobile Court Service) wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Kata ya Uyole Bi. Sikuzani Kibona


Maafisa Mahakama kutoka Idara ya Usimamizi wa Mashauri (DCM) na Viongozi wa Mahakama Kuu kutoka Masjala Ndogo ya Mbeya wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Watumishi wanaohudumu katika Mahakama inayotembea (Mobile Court Service), Nyuma yao ni Gari linalotoa huduma ya Mahakama inayotembea likiwa mbele ya jengo la mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho cha tathmini.

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho cha tathmini.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni