Jumatatu, 8 Juni 2026

MAHAKAMA KUU YAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA GEREZA KUU LA RUANDA MBEYA

Na. MUKSINI NAKUVAMBA, Mahakama Mbeya

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu amefanya ziara ya kutembelea Gereza Kuu la Ruanda jijini Mbeya hivi karibuni kwa ajili ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo, ikiwa ni zaira ya ukaguzi wa kawaida gerezani hapo katika kipindi cha Aprili –Juni, 2026.

Akiwasilisha taarifa fupi ya Gereza Kuu la Ruanda Mkuu wa Gereza Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Christopher Fungo, alieleza hali za wafungwa na mahabusu waliopo gerezani hapo.  

Katika ziara hiyo Mhe. Temu alipata fursa ya kukutana na Wafungwa na Mahabusu ambao waliwasilisha changamoto zao kwa viongozi mbalimbali wa Mahakama na wadau wengine wa haki jinai alioambatana nao katika ziara hiyo.

Katika risala yao wafungwa na mahabusu waliweza kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili gerezani hapo. Aidha Mhe. Temu aliahidi kuzishughulikia changamoto zote zilizowasilishwa katika risala zao na zile ambazo zipo nje ya uwezo kuziwasilisha katika mamlaka husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza Ruanda ACP Christopher Fungo alitoa shukurani zake kwa ujio wa ziara hiyo, kwa kuwa umekuwa na tija kubwa kwao kwa kutoa fursa kadhaa ikiwemo matendo ya huruma na kushughulikia suala la kupunguza mlundikano wa mahabusu gerezani hapo.

Katika ziara hiyo Mhe. Temu aliambatana na Viongozi mbalimbali wa Mahakama akiwemo Kaimu Mtendaji Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya Bw. Alintula Ngalile, Mahakimu Wakazi wakiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawadi Laizer, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mwenyekiti TLS Chapta ya Mbeya, Maafisa wa TAKUKURU, Ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Afisa Huduma na Uangalizi Mbeya na wadau wengine wa Haki jinai.

Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (wanne kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na viongozi wa Grezeza Ruanda na Mahakama kanda ya Mbeya na wadau wengine wa haki jinai alioambatana nao mbele ya Lango la Gereza Kuu Ruanda Mbeya. watatu kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Ruanda Mbeya Kamisha Msaidizi ACP Christopher Fungo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer (watano kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya, Mhe. Tedy Mlimba (wapili kulia).

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (aliyeketi mbele) na wadau wengine wa haki jinai alioambatana nao katika ziara hiyo wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya. Aliyesimama ni Mkuu wa Gereza Kuu la Ruanda Mbeya Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Christopher Fungo.


Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (kulia) akilakiwa na Mkuu wa Gereza Kuu la Ruanda Mbeya Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Christopher Fungo (kushoto) wakati wa ziara hiyo

Viongozi wa Mahakama na Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali za haki jinai walioshiriki katika ziara hiyo wakiwa Mbele ya kasha linalotoa huduma ya mahakama mtandao Gereza Kuu Ruanda

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (wa kwanza aliyeketi kushoto) na wadau wengine wa haki jinai alioambatana nao katika ziara hiyo wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya. Aliyesimama ni Mkuu wa Gereza Kuu la Ruanda Mbeya Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Christopher Fungo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni