Bw. Renatus Mlingi enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Renatus Mlingi aliyekuwa Dereva Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Iringa.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Iringa, Bi. Melea Mkongwa, marehemu Renatus amefariki dunia jana tarehe 06 Juni, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo ndipo alipokuwa akitibiwa awali.
Bi. Melea amesema kuwa, Marehemu Bw. Renatus anatarajiwa kuzikwa Iringa Mjini siku ya Jumanne tarehe 09 Juni, 2026.
Marehemu Renatus alizaliwa tarehe 21 Januari, 1974 na aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe 01 Oktoba, 2013 kwa Kada ya Dereva Daraja II.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu Renatus Mlingi.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni