Alhamisi, 18 Juni 2026

JAJI FAHAMU MTULYA AAGWA MUSOMA KUFUATIA UHAMISHO WA KITUO

  • Yamkaribisha pia Jaji Kakolaki katika Kituo hicho

Na FRANCISCA SWAI, Mahakama-Musoma

Uongozi na watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo Musoma wamejumuika kumuaga Jaji Fahamu Mtulya kufuatia uhamisho wake kwenda Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya na kumkaribisha Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki aliyehamia kutokea Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mtwara.

Hafla ya kumuaga Jaji Mtulya na kumkaribisha Jaji Kakolaki ilifanyika tarehe 14 Juni, 2026 katika Viwanja vya Mahakama Kuu Musoma.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtulya aliwashukuru watumishi na wadau wote wa Mahakama Musoma kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake akiwa Musoma.

Pia, aliwaasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa umoja na upendo, kuzingatia maadili ya kazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Zaidi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau katika kuhakikisha shughuli za Mahakama zinafanyika kama inavyopaswa.

Naye Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki aliwashukuru Uongozi, watumishi na wadau wote wa Mahakama Kanda ya Musoma kwa kumkaribisha na kuahidi kutoa ushirikiano pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wao watumishi wa Mahakama Kuu Musoma walimshukuru Jaji Mtulya kwa uongozi wake thabiti, malezi bora kwa watumishi wa kada zote, kuwa mfano hai wa mchapakazi, uadilifu, upendo na kujitoa kwake katika kazi, matukio ya kijamii, kuhamasisha umoja, michezo na utalii wa ndani.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi, Mkuu wa Wilaya Musoma, Mhe. Juma Chikoka pamoja na Wadau mbalimbali wa Mahakama ambao wote kwa pamoja walitoa salamu na zawadi mbalimbali kumshukuru Jaji Mtulya kwa uongozi wake imara uliothibitika kwa uwajibikaji, uadilifu, na mashirikiano mzuri na wadau.

 Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili kushoto) akijiandaa kukata keki na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati)wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Mtulya na kumkaribisha Jaji Kakolaki (katikati). Wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Musoma, Mhe. Marlin Komba, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Musoma, Mhe. Kamazima Idd na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Kanali Evans Mtambi.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Musoma, Mhe.Edwin Kakolaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Kanali Evans Mtambi (kulia).

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akipokea mkono wa kwaheri kutoka kwa Chama cha  Mahakimu na Majaji (TMJA) Tawi la Musoma.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Musoma.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili kushoto) akiwa ameshika zawadi aliyopatiwa ikiwa ni ishara ya shukrani na kumtakia kheri kutoka kwa Viongozi wa Mahakama Kuu Musoma ambao ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Omari Kingwele (wa kwanza kushoto), wa pili kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma,  Mhe. Monica Ndyekobora na wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama Masjala Ndogo ya Musoma, Bw. Leonard Maufi.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akipokea zawadi ikiwa ni ishara ya mkono wa kwaheri na shukrani kutoka kwa watumishi ambao ni wadau wa utalii Masjala ndogo Musoma.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya hafla ya kumuaga ambao ni watumishi wa Kanda ya Musoma.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla ya kumuaga.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (kulia) akipokea mkono wa kwaheri na shukrani kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Musoma, Mhe. Juma Chikoka.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akipokea mkono wa kwaheri na shukrani kutoka wadau wa Mahakama kwa namna alivyokuwa mstari wa mbele kuhamasisha shughuli za utalii wa ndani.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni