Na ARAPHA RUSHEKE, Mahakama Kuu Dodoma.
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Biswalo Mganga,
amewaongoza Watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma katika hafla fupi ya kumpongeza
Mhe. Zabibu Mpangule, mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Naibu Msajili
wa Mahakama Kuu Dodoma.
Hafla
hiyo imefanyika tarehe 17 Juni 2026 katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji
Haki (IJC) Dodoma.
Akizungumza
kwa niaba ya watumishi, Mhe. Mganga amempongeza Mhe. Mpangule kwa kuaminiwa na
kupewa nafasi hiyo muhimu, akieleza kuwa uteuzi wake ni matokeo ya utendaji
kazi uliotukuka, uadilifu na kujituma katika kutekeleza majukumu yake.
Kabla
ya uteuzi huo, Mhe. Mpangule alikuwa akihudumu kama Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo alitoa mchango mkubwa katika utoaji wa
huduma za haki kwa Wananchi.
Kwa
upande wake, Mhe. Mpanguke aliwashukuru Watumishi kwa pongezi zao na kuhahidi
kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kujituma kwa manufaa
ya Mahakama na Wananchi kwa ujumla.
Watumishi
wa Mahakama Kuu Dodoma pamoja na Wilaya zake walimtakiwa kila la kheri katika
majukumu yake mapya.
Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na kumpatia dhawadi Naibu Msajili mteule (wa nne kutoka kushoto).

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni