Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, leo tarehe 17 Juni, 2026
amewaapisha Naibu Wasajili 31 wapya wa Mahakama ya Tanzania aliowateua hivi
karibuni.
Hafla ya uapisho huo
imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini
Dodooma. Uapisho huo unafanya jumla ya Naibu Wasajili wanaohudumu katika
Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani kufikia 108.
Viongozi mbalimbali wa
Mahakama, akiwemo Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George
Masaju, wamehudhuria hafla hiyo. Wengine ni Majaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Amir
Mruma na Mhe. Biswalo Mganga, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva
Nkya na Kaimu Mtendaji Mkuu na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Victor
Kategere.
Wengine ni Msajili wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Chiganga
Tengwa, Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni, Bi. Mary Shirima, Mtendaji wa
Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu,
Mhe. Sundi Fimbo.
Viongozi wengine ni Menejimenti
ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, Naibu
Wasajili, Watendaji wa Mahakama, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wa
Mahakama, Wazazi, Wenza, ndugu na jamaa wa Naibu Wasajili wapya.
Walioapishwa kwenye hafla
hiyo ni Mhe. Agnes Lawrence Mchome kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Richard
Eustace Kabate kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Janeth Elias Masesa kutoka
Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, Mhe. Ushindi Solomon Swallo kutoka Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Charles Tumaini Mnzava kutoka Mahakama ya Hakimu
Mkazi Mtwara.
Wengine ni Mhe. Cleofas
Frank Waane kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mhe.
Liad Mohamed Chamshama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, Mhe.
Hassan Ahmed Makube kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe.
Mariam Bakari Lusewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mhe. Joyce
Josephat Mkhoi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha.
Kwenye orodha wapo pia Mhe.
Consolata Peter Singano kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. Glory
Gabriel Mwakihaba kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe.
Mkama Ally Abdallah kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Moshi, Mhe.
Allu Omary Nzowa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida na Mhe.
Zabibu Abeid Mpangule kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.
Wengine ni Mhe. Asha
Hassani Waziri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mhe.
Erick Robert Marley kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Mhe. John Calist
Msafiri kutoka Mahakama ya Wilaya katika Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Geofrey
Jeremia Mhini kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Gway Kwaslema
Sumaye kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.
Wapo pia Mhe. Gabriel
Patrick Ngaeje kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, Mhe. Zawadi David Laizer
kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Martha Mahumbuga kutoka Mahakama ya
Hakimu Mkazi Simiyu, Mhe. Kisasila Malangwa Saguda kutoka Mahakama ya Hakimu
Mkazi Sumbawanga na Mhe. Erasto Jacobo Philly kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha.
Wengine ni Mhe. Japheti
Bwire Manyama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Mhe.
Is-Haq Bakari Kuppa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mhe.
Samwel Obasi Josiah kutoka Mahakama ya Wilaya Malinyi, Mhe.
Jasmini Abdul Athuman kutoka Mahakama ya Wilaya Siha, Mhe. Mwanaheri Kassim
Rashid kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Tanga na Mhe. Domician Denice Mlashani kutoka
Makao Makuu ya Mahakama.































Hakuna maoni:
Chapisha Maoni