Jumatano, 17 Juni 2026

JAJI MFAWIDHI AHITIMISHA ZIARA YA UKAGUZI MBEYA

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya.

·        Amepongeza jitihada zinazofanywa kulinda miundombinu ya Mahakama mpya za mwanzo.

·        Amepongeza Serikali za Kata na Vijiji kwa ushirikiano wao katika kuboresha miundombinu ya Mahakama kwa kusaidia ukarabati na hata kutoa Majengo yao kwa matumizi ya Mahakama.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga amehitimisha ziara ya siku kumi za ukaguzi ulioanza mwanzoni mwa mwezi Juni 2026 kwa kutembelea Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo Mbarali, Chunya, Kyela na Rungwe zilizopo Masjala Ndogo ya Mbeya.

Lengo la ukaguzi huo ni kukumbushana juu ya majukumu ya kila siku, kubaini, mapungufu na changamoto na kuona mapendekezo ya njia sahihi za kukabiliana na changamoto hizo.

Katika vikao mbalimbali vilivyofanyika wakati wa ziara hiyo Mhe. Tiganga aliwasisitiza watumishi kuongeza kasi katika usikilizwaji wa mashauri, kudumisha nidhamu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kudumisha ushirikiano kazini.

“Ninawapongeza kwa kuendelea kudumisha nidhamu, tuendelee kuchapa kazi, tutunze maadili yetu na ninawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya na ninawatakieni kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yenu,” alisema Mhe. Tiganga.  

Aidha, Mhe. Tiganga alizipongeza Serikali za Kata na vijiji na wananchi wa maeneo hayo kwa ushirikiano wao mzuri kwa kuisaidia Mahakama kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusaidia katika harakati za ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Makongorosi iliyopo wilaya ya Chunya na kupatiwa Jengo kwa ajili ya matumizi ya Mahakama ya Mwanzo Ilongo wilayani Mbarali.

Katika ziara hiyo Mhe. Tiganga aliongozana na viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya ambao ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawad Laizer.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya Wilaya Rungwe

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Chunya.

Sehemu ya watumishi wakimsikiliza Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (hayupo pichani) akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya mwanzo Chimala –Mbarali



Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer, wakipanda mti wa matunda kwa Pamoja katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Madibira- Mbarali.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya mwanzo Madibira –Mbarali

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akipanda mti wa matunda katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Madibira- Mbarali.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti akipanda mti wa matunda katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Ndobo Kyela.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye moja ya vikao katika ziara hiyo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.



Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akisaini kitabu cha wageni na baadae akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni