Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Bukoba
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Bukoba,
Mhe. David Ngunyale, hivi karibuni alifanya ziara katika Mahakama ya Wilaya Kyerwa
kwa lengo la kujitambulisha.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Ngunyale aliwataka
Watumishi wa Mahakama hiyo kuendelea kukumbatia maendeleo yaliyopatikana katika
utoaji haki na kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kuwafikia wananchi
wengi zaidi kutoa huduma iliyo bora.
Jaji Ngunyale amekumbushia umuhimu kujiendeleza kielimu ili
kuongeza ufanisi katika majukumu ya utoaji haki. Amesisitiza utoaji haki
uendane na ubora unaohitajika kuweza kufikia malengo ya Mahakama.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba, Mhe. David Ngunyale (katikati) akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Kyerwa. Kulia kwakwe ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Bukoba, Mhe. Saidi Mkasiwa na kushoto kwakwe ni Kaimu Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Allen Ifunya.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba, Mhe. David Ngunyale na Naibu Msajili Mahakama Kuu Bukoba, Mhe. Saidi Mkasiwa wakifatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu iliyokuwa inasomwa na Kaimu Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Allen Ifunya.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba,
Mhe. David Ngunyale (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya
pamoja na Watumsihi wa Mahakama ya Wilaya Kyerwa. Wengine waliokaa kuanzia
kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Bukona, Mhe. Saidi Mkasiwa na Kaimu
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilya Kwerw, Mhe. Allen Ifunya.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba,
Mhe. David Ngunyale akionyeshwa maeneo mbalimbali ya Mahakama
ya Wilaya Kyerwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni