Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Mtwara
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina
Mteule, hivi karibuni amefanya ziara ya ukaguzi na kutembelea Gereza Kuu la
Lilungu katika Mkoa wa Mtwara, ili kujionea utendaji kazi wa Gereza hilo.
Ziara
hiyo ilijumuisha pia mazungumzo ya pamoja na Askari Magereza na kufanya ukaguzi
wa mazingira na kupata taarifa za utendaji kazi, mafanikio na changamoto.
Aidha,
Jaji Mfawidhi pia alizungumza na kusikiliza changamoto za Wafungwa, mawazo na
maoni kutoka kwa Watumishi kutoka kwa Wadau.
Mhe.
Mteule aliahidi kujibu changamoto ambazo zilizokuwa katika meza yake kwa upande
wa Mahakama, na kuwaomba kila mmoja kuweza kushiriki utendaji kazi bora katika
maeneo yanayohusu Magereza.
Aliwasisitiza
matumizi ya TEHAMA kwa wale ambao mashauri yao bado kwenye kusikilizwa na
kuhakikisha kunakuwa na uwezekano wa kupunguza gharama za kila mara.
Katika ziara hiyo, Jaji Mfawidhi aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mtwara, Mhe. Seraphine Nsana, Mtendaji wa Mahakama Mtwara, Bw. Yusuph Msawanga na Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mfawidhi, Mhe. Stella Shindika.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule, akipokelewa na Askari Magereza
wakati wa ziara yake.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule, akipata picha ya
pamoja na Askari Magereza pamoja na Wadau mbalimbali.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule, (katikati) akipata
picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara ya
ukaguzi.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Singida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni