- Jaji Kihwelo asisitiza uadilifu
Na
ARAPHA RUSHEKE, Mahakama Kuu Dodoma.
Jaji
wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi
wa Mahakama Lushoto, amehitimisha mafunzo ya siku tatu yaliyolenga kuimarisha
uwezo wa Mahakimu katika kushughulikia mashauri ya unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia kwa kuzingatia utu, heshima na ustawi wa waathirika.
Akifunga
mafunzo hayo tarehe 24 Juni, 2026 yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano
kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma, Mhe. Dkt. Kihwelo alisisitiza
umuhimu wa Mahakimu kuzingatia uadilifu, weledi na misingi ya haki wakati wa
kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha waathirika
wanapata haki bila kuongeza maumivu ya kisaikolojia.
Jaji
Kihwelo alisema mafunzo hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kujifunza, kubadilishana
uzoefu na kuimarisha uelewa wa namna bora ya kuhudumia waathirika wanaofika
mahakamani kutafuta haki. Aliwataka washiriki kutumia maarifa waliyojifunza
katika utendaji wao wa kila siku ili kuendelea kujenga imani ya wananchi kwa
mhimili wa Mahakama.
Kwa
upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga,
aliwashukuru wawezeshaji na washiriki kwa ushiriki wao mzuri na kusisitiza
umuhimu wa kuendeleza mafunzo ya aina hiyo ili kuongeza ufanisi katika utoaji
wa haki kwa makundi yenye uhitaji maalum.
Mafunzo
hayo yalihitimishwa kwa ugawaji wa vyeti kwa washiriki, zoezi lililoongozwa na Jaji
Kihwelo, kabla ya Viongozi na washiriki kupiga picha ya pamoja kuashiria
kufungwa rasmi kwa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuimarisha utoaji wa haki unaozingatia utu wa binadamu, kuongeza uadilifu na weledi katika usikilizaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuimarisha ulinzi wa haki za waathirika ndani ya mfumo wa Mahakama.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt Paul
Kihwelo, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya unyanyasaji wa kijinsia. .
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Mhe, Dkt Paul Kihwelo, (aliyekaa katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo hayo. Aliyeketi kushoto kwake ni
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe Joachim Tiganga. Kulia ni Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe Upendo Ngitiri.
Meza
kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, ambaye pia ni
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe, Dkt Paul Kihwelo (aliyekaa katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki. wa mafunzo hayo. Aliyeketi kushoto
kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, kulia ni
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri.
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe, Dkt Paul Kihwelo, (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. Aliyeketi kushoto kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe Joachim Tiganga, kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Singida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni