- Asisitiza uadilifu, weledi, uwajibikaji
Na
ARAPHA RUSHEKE, Mahakama Kuu Dodoma.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
ya Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, ameanza rasmi majukumu yake kwa kukutana na Watumishi wa Kituo
Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) mara baada ya kuripoti katika kituo hicho.
Katika ziara hiyo aliyoifanya tarehe
22 Juni, 2026, Mhe. Tiganga alitembelea kila ofisi ya mtumishi ili kujionea mazingira ya
kazi na kufahamu kwa karibu shughuli zinazotekelezwa na watumishi.
Baadaye, Mhe. Tiganga alifanya kikao na wawakilishi wa watumishi pamoja na wakuu wa
vitengo mbalimbali vya Mahakama katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma.
Katika
kikao hicho, alieleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha utendaji kazi,
ushirikiano na utatuzi wa changamoto zinazoweza kujitokeza katika mazingira ya
kazi.
Aidha,
Jaji Mfawidhi alisikiliza maoni, ushauri na hoja mbalimbali kutoka kwa
watumishi, akisisitiza umuhimu wa mawasiliano ya wazi, uwajibikaji na
mshikamano ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.
Akihitimisha kikao hicho, aliwahimiza watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma, huku akiahidi kushirikiana nao katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utendaji wa Mahakama na huduma kwa umma.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa katikati) akisema neno wakati wa kikao chake na watumishi waliopo IJC Dodoma, kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri na kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Bw.Bedson Mariba.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma waliohudhuria kikao hicho.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma waliohudhuria kikao hicho.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma waliohudhuria kikao hicho.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma waliohudhuria kikao hicho.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni