Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Mtwara
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule,
hivi karibuni amefanya ziara ya ukaguzi wa Mahakama za Mkoa wa Mtwara ili
kujionea utendaji kazi ili kuhakikisha huduma ya utoaji haki inaendelea kufanya
vyema.
Miongoni
mwa Mahakama zilizokaguliwa ni Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya
Tandahimba, Newala, Nanyumbu, Masasi na Mahakama za Mwanzo Litehu,
Mnyambe, Nakopi, Chiungutwa.
Ziara
hiyo pia ilijumuisha mazungumzo ya pamoja na Watumishi wa Mahakama alizopita
kwa ajili ya ukaguzi. Aliweza kupata taarifa za utendaji kazi, mafanikio,
changamoto, mapato na matumizi.
Mhe.
Mteule aliwapongeza Mahakimu na Watumishi wa Mahakama kwa utendaji bora na
mzuri, hasa kumaliza mashauri kwa wakati, kutokuwa na mlundikano.
Katika
ukaguzi huo pia, Jaji Mfawidhi aliwapongeza Watumishi wa Mahakama katika
matumizi wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo
inawezesha kufuatilia na kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao. Aliwasisitiza
kuendelea kuwaelewesha Wananchi kwenye matumizi ya mifumo hiyo ili kupunguza
gharama za kila mara.
Katika
ziara hiyo, Jaji Mfawidhi aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mtwara,
Mhe. Seraphine Nsana, Mtendaji wa Mahakama Mtwara, Bw. Yusuph Msawanga na
Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mfawidhi, Mhe. Stella Shindika.
Jaji Mfawidhi pia alitembelea na kukagua Mahakama ya Wilaya Masasi iliyopo katika ujenzi na kusisitiza ufanyike kwa kuzingatia ubora na kwenda kwa wakati.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule akisalimiana
na Mahakimu na Watumishi katika Mahakama ya Wilaya Newala.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule,
akipanda mti wa ukumbusho katika Mahakama ya Wilaya Newala.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule
akiwa katika ukaguzi wa eneo la Mahakama ya Mwanzo Mnyambe iliyopo Wilaya ya
Newala.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule (kushoto mbele) akiwa kwenye ukaguzi wa eneo la Mahakama ya Mwanzo Litehu.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule
(katikati) akipata picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo
Chiungutwa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo
Litehu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Nakopi.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Singida.














Hakuna maoni:
Chapisha Maoni