Marehemu Angela Angelus Mtesigwa enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bi. Angela Angelus Mtesigwa aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Simiyu kama Mwandishi Mwendesha Ofisi.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Simiyu, Bw. Gasto Kanyairita marehemu Angela alifikwa na umauti Alfajiri ya tarehe 26 Juni, 2026 katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.
Bw. Kanyairita amesema, mazishi yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 29 Juni, 2026 Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Mahakama ya Tanzania inaungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni