Jumapili, 21 Juni 2026

JAJI MFAWIDHI MPYA DODOMA ATAMBULISHWA KWA MKUU WA MKOA

Na ARAPHA RUSHEKE- Mahakama Kuu Dodoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, tarehe 19 Juni 2026, alimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, kwa ajili ya kutambulisha.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni siku moja tu tangu Mhe. Tiganga aliporipoti rasmi katika kituo chake kipya cha kazi baada ya kuhamishwa kutoka Mahakama Kuu Mbeya.

Katika ziara hiyo, Mhe. Tiganga aliambatana na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Juliana Masabo. Mhe. Dkt.Masabo akitumia fursa hiyo kumuaga Mkuu wa Mkoa.

Pande hizo mbili zilijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Mahakama na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kuhakikisha huduma za haki zinaendelea kutolewa kwa ufanisi na kwa manufaa ya Wananchi.

Mkuu Mkoa alimkaribisha Mhe. Tiganga na kumtakia mafanikio mema katika majukumu yake mapya, huku akiahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Taasisi hizo muhimu.


Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt Juliana Masabo, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe, Rosemary Senyamule (aliyepo katikati) akizungumza na wageni kutoka Mahakama ya Tanzania mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake Jijini Dodoma.


 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe, Rosemary Senyamule (aliyepo katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Mahakama mara baada ya kumtembelea ofisini kwake. Kulia kwake ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt Juliana Masabo na aliyepo kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma Mhe Joachim Tiganga.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe, Rosemary Senyamule (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Mahakama pamoja na Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wa tatu kutoka kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Juliana Masabo na wa tano kutoka kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, wa sita kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe/ Upendo Ngitiri na wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Dodoma Bw. Bedson Mariba.

 

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Songea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni