Na KANDANA LUCAS-Mahakama Kuu, Musoma
Makabidhiano ya Ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma, yamefanyika hivi karibuni, kufuatia uhamisho wa mtangulizi wake, Mhe. Fahamu Mtulya kwenda Mahakama Kuu Mbeya.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Mtulya aliwashukuru Watumishi wa Mahakama Musoma
kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha utumishi wake. Alisema mafanikio yaliyopatikana yametokana
na ushirikiano mzuri kati ya Viongozi na Watumishi, kujituma na uwajibikaji katika
kutekeleza majukumu yao.
Aidha,
Mhe. Mtulya aliwaasa Watumishi kuendeleza kudumisha mshikamano na kumpatia
ushirikiano Jaji Mfawidhi mpya, Mhe. Edwin Kakolaki, ili kuhakikisha huduma za
kimahakama zinaendelea kutolewa kwa ufanisi.
Kwa
upande wake, Mhe. Kakolaki aliahidi kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na
mtangulizi wake pamoja na kushirikiana na Watumishi wote katika shughuli za
utoaji haki kwa Wananchi.
Vilevile
Mhe, Jaji Mfawidhi mpya aliwahimiza Viongozi wote na Watumishi kuendelea
kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa
umma.
Makabidhiano
hayo yalihusisha taarifa za utendaji kazi, hali ya mashauri, vifaa vya kazi
pamoja na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Mahakama Musoma.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki,
akisalimiana na Watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma baada
ya kuwasili kushiriki makabidhiano ya ofisi.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Songea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni