Na. ELIUD KIWANGA – Mahakama, Songwe
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Songwe
Mhe. Gabriel Pascal Malata aongoza hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo Kanga
iliyopo Kata ya Kanga, Wilaya ya Songwe hivi karibuni
Hafla hiyo, ilifanyika katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo
Kanga na ilihudhuriwa na sehemu ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa wa Songwe pamoja
na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim
Charles Tiganga, Naibu
Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu pamoja na Mtendaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Marvis Miti.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Katibu wa Mbunge wa
Jimbo la Songwe Bw. Agapto Thomas Kilongosi alitoa pongezi kwa Mahakama ya
Tanzania kwa kuendelea kuimarisha huduma za upatikanaji wa haki ikiwa ni pamoja
na kukamilisha ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kanga na kuahidi kuendelea
kushirikiana na Mahakama katika kuboresha upatikanaji wa haki katika Jimbo la Songwe.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kanga Bw. Prosper Laurent Nkinga, aliishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kusogeza huduma ya Mahakama katika Kata ya Kanga na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kulinda miundombinu ya Mahakama hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Fadhili
Nkurlu aliishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kusogeza huduma ya
upatikanaji wa haki katika Kata ya Kanga na maeneo ya Jirani kwa kujenga Mahakama
ya Mwanzo Kanga.
Mhe. Fadhili
Nkurlu aliahidi
kuendelea kushirikiana na Mahakama ikiwa ni pamoja na kulinda miundombinu ya Mahakama
ili kuhakikisha huduma za utoaji wa haki zinatolewa ipasavyo katika Mahakama ya
Mwanzo Kanga na Wilaya ya Songwe kwa ujumla.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Omari Makame
alimshukuru Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim
Charles Tiganga kwa ushirikiano aliouonesha wakati Mkoa wa Songwe
ulipokuwa ukipata huduma za Mahakama kutoka Masjala Ndogo ya Mbeya, Pia
alimkaribisha Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel
Pascal Malata na aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufikisha huduma ya
upatikaji wa haki kwa wanachi wa Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa huyo akatumia jukwaa hilo kumshukuru Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja Jaji Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Goerge Masaju kwa maono yao ya kuendelea kuboresha
miundombinu ya Mahakama ya Tanzania, Pia aliwaomba na kuwahimiza wananchi wa Kanga
na Songwe kwa ujumla kuilinda na kuitunza miundombinu ya Mahakama kwa sababu
imejengwa ili kusogeza huduma ya upatikanaji wa haki katika maeneo yao.
Vilevile, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga alipongeza uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo Kanga na
alishukuru kwa ushirikiano alioupata wakati Mkoa wa Songwe ulivokuwa ukipata
huduma kutoka Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, pia alipongeza Mahakama ya
Tanzania kwa kusogeza huduma ya Makama Kuu na Mahakama ya Rufani kwa kuanzisha Mahakama
Kuu Masjala Ndogo ya Songwe.
Naye, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe
Mhe. Gabriel Pascal Malata alieleza kuwa, Mahakama ya Mwanzo Kanga imejengwa
ili kusogeza huduma ya utoaji wa haki katika Kata ya Kanga na maeneo ya jirani
pia aliwataarifu wananchi kwamba, huduma za Mahakama kuanzia ngazi ya Mahakama
ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani
zinatolewa na kupatikana ndani ya Mkoa wa Songwe.
Mhe. Malata alisisitiza kwamba, wananchi wote
wanawajibika kulinda na kutunza miundombinu ya Mahakama kwa sababu ni mali ya
umma na imejengwa kwa kodi za wananchi, pia Mhe. Malata aliwapongeza wananchi
wa Kanga kwa kusimama kidete kuitunza na kuilinda Mahakama ya Kanga ilipotaka
kuchomwa moto mwezi Oktoba mwaka jana.
Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (katikati) akiwa katika
hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo Kanga, wengine (wa kwanza kulia) ni Mkuu wa
Wilaya ya Songwe Mhe. Fadhili Nkurlu, (wa pili kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Omari Makame, (wa nne kutoka kulia) ni Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim
Charles Tiganga na (wa tano
kulia) ni Diwani wa Kata ya Kanga Bw. Prosper Laurent Nkinga.
Jaji Mfawidhi Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya
Songwe Mhe. Gabriel Malata akipanda mti wa kivuli katika viunga vya Mahakama ya
Mwazo Kanga baada ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa
Mahakama ya Mwanzo Kanga.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa kwanza kushoto), Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Makame (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Fadhili Nkurlu (wanne kushoto) na Katibu wa Mhe. Mbunge wa Jimbo la Songwe Bw. Agapto Kilongosi katika zoezi la kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahakama hiyo Mwanzo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya
Songwe Mhe. Gabriel Pascal Malata akihotubia wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya
Mwanzo Kanga.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo
ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akitoa neno katika hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya
Mwanzo Kanga.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Bw. Sostenes
January Mayoka akifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya
Mwanzo Kanga.
Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe
Mhe. Joyce Minde akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya uzinduzi wa Mahakama
ya Mwanzo Kanga.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni