Na. ALLY RAMADHANI – Mahakama, Katavi
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko hivi karibuni alifanya ziara ya kutembele
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Katavi katika ziara hiyo amefanikiwa
kutembelea mradi wa jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC).
Katika
ziara hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amefanikiwa kubaini changamoto ya umeme inayolitesa
jengo hilo la Mahakama, huku akitioa maelekezo kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Katavi kwa kumpatia masaa 48 (siku mbili) wawe wametatua changamoto hiyo.
“Changamoto
hii ya umeme katika jengo la Mahakama yetu sifurahishwi nayo, hivyo basi nampatia
siku mbili Meneja wa TANESCO Mkoa tatizo hili la umeme katika jengo letu la
Mahakama liwe limepatiwa jawabu,” alisema Mhe. Mwanamvua Mrindoko
Aidha,
kupitia ziara hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo
Katavi Mhe. Godfrey Ntemi Isaya, amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa kusema
“Tunatambua mchango wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa kufatilia upatikanaji
wa eneo hili na leo unakuja kutembelea jengo likiwa limekamilika tunashukuru
sana na nikupongeze kwa hilo”.
Hata
hivyo, Mhe. Isaya amemuomba Mkuu wa Mkoa swala la kupatiwa maeneo kwa ajili ya
uanzishwaji wa Mahakama za Mwanzo kutokana na jiografia ya Katavi ili huduma za
utoaji haki zisogezwe karibu na wananchi.
Pia
Jaji Mfawidhi hiyo, alisema kuwa, Mahakama ya Tanzania inasisitiza Utoaji Haki
kwa wakati mapema ipasavyo, hivyo basi Mahakama ya Tanzania inatekeleza mpango
huo kwa kuboresha mazingira ya utoaji haki na kusogeza huduma za utoaji haki
karibu zaidi na wananchi kwa kujenga miundombinu bora.
Kupitia
ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi amewatangazia wananchi wa Katavi kuwa huduma
za Mahakama Kuu zimeanza mkoani hapo tangu tarehe 30 Machi, 2026, hivyo wananchi
wasisumbuke kwenda Sumbawanga kwa kufuata huduma za Mahakama Kuu wakati Katavi
wanatoa huduma hizo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo Katavi, Mhe Godfrey
Ntemi Isaya akitoa taarifa fupi wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe Mwanamvua Mrindoko akisalimiana na watumishi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Katavi wakati wa ziara yake alipotembelea Mahakama kuu Katavi.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni