Jumatatu, 15 Juni 2026

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU MTWARA AHAMIA MUSOMA

Na MWANDISH WETU-Mahakama, Mtwara

Jaji Mfawidhi wa zamani wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki, amehamishiwa Musoma kwenda kuendelea na wadhifa huo.

Tarehe 12 Juni, 2026, Mhe. Kakolaki alikabidhi ofisi kwa Jaji Mfawidhi mpya wa Masjala hiyo, Mhe. Katarina Mteule ambaye ametokea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Tanga.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Mahakama, akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Mtwara, Mhe. Said Ding’ohi, Naibu Msajili, Mhe. Seraphine Nsana, Mhe. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkawzi Mtwara, Mhe. Tumaini Mnzava pamoja na Mtendaji wa Mahakama Mtwara, Bw. Yusuph Msawanga.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mhe. Mteule alieleza kufurahishwa na mapokezi aliyoyapata kutoka kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Mtwara.

“Nawashukuru kwa mapokezi mazuri na upendo wa kipekee mlionionesha. Naomba tushirikiane kwa karibu katika jukumu letu la utoaji haki kwa jamii kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na furaha,” alisema Mhe. Mteule.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule, (kushoto) akipokelewa na Jaji Edwin Kakolaki. Katikati ni Mhe. Jaji Saidi Ding'ohi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule (katikati0 akisalimiana na Mtendaji wa Mahakama Mtwara baada ya kuwasili.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule (katikati0 akisalimiana na Watumishi wakati wa mapokezi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule (kushoto) na Jaji Edwin Kakolaki (kulia) wakiwa katika ofisi ya Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Mtwara.

Jaji Mfawidhi Edwin Kakolaki (kushoto) na Mhe. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, Mhe. Katarina Mteule, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiana ofisi.

Majaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto), Mhe. Katarina Mteule (katikati) na Mhe. Said Ding'ohi (kulia) wakiwa kwenye kikao na Watumishi wa Mahakama Kuu Mtwara baada ya mapokezi.

Mahakimu pamoja na Watumishi wengine katika kikao baada ya mapokezi ya Jaji Mfawidhi Katarina Mteule.

Naibu Msajili, Mhe. Seraphine Nsana (kushoto), Mhe. Edwin Kakolaki (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi Katarina Mteule (katikati), Mhe. Said Ding'ohi (wa pili kulia) na Mtendaji wa Mahakama Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mahakama Kuu Kanda Mtwara.  

Jaji Edwin Kakolaki (kushoto), Jaji Mfawidhi Katarina Mteule (katikati) na Jaji Said Ding'ohi (kulia walioketi), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu wa Mahakama Mtwara.

Jaji Edwin Kakolaki (kushoto), Jaji Mfawidhi Katarina Mteule (katikati) na Jaji Said Ding'ohi (kulia walioketi), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni