TANZIA
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bw. Ramadhani Magania maarufu kama Jumbe ambaye alikuwa Dereva wa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mahakama ya Tanzania kilichotokea ghafla usiku wa leo Jumapili tarehe 14 Juni, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Juni, 2026 na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick marehemu Ramadhani amefikwa na umauti leo Jumapili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Bi. Beatrice amesema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu Ramadhani Magania.
HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE YEYE TUTAREJEA (INNA LILLAH WA INNA ILLAH RAJIUN).


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni