Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 26 Juni, 2026 amemuapisha Dkt. John Antony Jingu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Dkt. Jingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mtangulizi
wake Mtendaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel. Hafla
hiyo fupi ya Uapisho imefanyika kwenye ukumbi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237, Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ndiye Katibu wa Tume na Mtekelezaji wa Maamuzi ya Tume hiyo.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni Chombo kilichoundwa kusimamia utendaji kazi wa Mahakama
ya Tanzania.
Mamlaka ya Tume ya
Utumishi wa Mahakama kama Chombo cha kusimamia ajira na nidhamu za Watumishi wa
Mahakama yanatokana na Ibara ya 113(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 29(1) cha Sheria ya Usimamizi
wa Mahakama.
Matukio katika
picha-Uapisho wa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Dkt. John Antony
Jingu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (kulia) akisaini hati ya kiapo cha Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 26 Juni, 2026. Anayeshuhudia ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.George Masaju.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.George Masaju akisaini hati ya kiapo cha Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Dkt. John Antony Jingu aliyeapishwa leo tarehe 26 Juni, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.George Masaju (kushoto) akimpongeza Dkt. John Antony Jingu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ambaye amemuapisha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 26 Juni, 2026 kwenye ukumbi wa Tume hiyo. Anayeshuhudia ni Bi. Enziel Mtei, Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (Ajira na Uteuzi).
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. John Antony Jingu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ambaye amemuapisha leo tarehe 26 Juni, 2026 kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (kushoto) ambaye ameapishwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Kulia ni Mtendaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama na aliyekuwa Katibu wa Tume hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel.













Hakuna maoni:
Chapisha Maoni