Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya amefanya
mazungumza na wadau wa haki jinai na madai wa Masjala Ndogo ya Mbeya kwa lengo
la kujitambulisha na kutambuana baina ya wadau hao kufuatia mabadiliko ya uongozi
katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika jana tarehe 23 Juni, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Mtulya aliwaasa wadau kudumisha
ushirikiano uliopo baina yao na Mahakama mbali na masuala ya kiofisi hata
katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo.
Kwa
upande wake, Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe.
Aziza Temu alitumia nafasi hiyo kuwaaga wadau hao kufuatia uhamisho wake wa kwenda
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam huku akiwashukuru wadau
hao kwa kuwa kinara wa kuhakikisha kuwa mashauri yanayamalizika mahakamani
mapema ipasavyo kupitia ushirikiano wao wa karibu na Mahakama.
Naye,
Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo alitoa
pongezi zake kwa wadau hao kwa namna walivyokuwa na ushirikiano mzuri kwa
Mahakama na kutumia nafasi hiyo pia kuwaaga kufuatia uhamisho wake wa kuhamia
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Morogoro.
Nao
wadau wa Mahakama waliahidi kudumisha ushirikiano uliopo baina yao na kueleza
matumaini yao juu ya usimamizi thabiti kutoka kwa viongozi wa Mahakama huku
wakitoa shukrani zao kwa Waheshimiwa Naibu Wasajili kwa muda wote walioshirikiana
kwa pamoja katika shughuli mbalimbali za kiofisi na kijamii hadi kufikia
uhamisho wao kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.
Aidha
Mhe. Mtulya alihitimisha kikao hicho kwa kuahidi kushughulikia changamoto zote
zilizowasilishwa na kuahidi kuwa mlezi bora kwa kuwajenga na kuwaweka katika
mstari mnyoofu ili kufanikisha malengo ya kutoa haki kwa wakati mapema ipasavyo
ili kukidhi matamanio ya wananchi wanaowahudumia.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya (aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa kikao chake na Wadau wa Mahakama wa haki jinai na madai, kikao kilichofanyika jana tarehe 23 Juni, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Kulia ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Aziza Temu na kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo.
Sehemu ya wadau wa haki jinai na madai waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali katika kikao hicho.
Mmoja wa wadau akizungumza na kuchangia mada kuhusu eneo lake la kazi katika kikao hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni