Na DOTTO NKAJA –Mahakama, Geita
Uongozi
na Watumishi wa Mahakama Kuu Masjla Ndogo Geita hivi karibuni walifanya hafla ya kumuaga aliyekuwa Jaji
Mfawidhi, Mhe. Kevin Mhina, kufuatia uhamisho wake wa kwenda kutekeleza
majukumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara.
Hafla
hiyo ilifanyika Juni 10, 2026, katika Viwanja
vya Mahakama Kuu Geita. Akizungumza
katika hafla hiyo, Mhe. Mhina aliwashukuru wote
kwa
ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake. Alisema
amefurahishwa na maandalizi ya hafla hiyo na kupongeza mshikamano ulioonyeshwa
na Watumishi.
Aidha,
aliwahimiza kuendelea kuzingatia maadili ya kazi, ushirikiano, utu na
uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Pia alisisitiza
umuhimu wa kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
ili kuimarisha utoaji wa huduma za haki na kuifanya Mahakama Geita kuwa mfano katika matumizi ya
teknolojia ndani ya Mhimili
wa Mahakama.
Kwa
niaba ya watumishi, Jaji wa Mahakama Kuu
ya
Tanzania, Mhe. Griffin Mwakapeje, alimpongeza Mhe. Mhina kwa mchango wake
mkubwa katika maendeleo ya Mahakama Geita, hususan katika kusimamia uanzishwaji
wa Masjala ya Mahakama Kuu Geita.
Alisema
uongozi wake wenye maono, uthabiti na kujitolea umechangia kuimarika kwa huduma
za Mahakama na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki kwa Wananchi.
Naye
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna, alimpongeza Mhe.
Mhina kwa juhudi zake katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya TEHAMA
katika shughuli za Mahakama.
Alisema
maarifa, uongozi na moyo wake wa kusaidia wengine vimechangia kwa kiasi kikubwa
kuboresha matumizi ya teknolojia katika uendeshaji wa mashauri, usikilizaji wa
kesi na shughuli za kiutawala.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa Mahakama Geita, Bi. Masalu Kisasila, alisema Mhe.
Mhina ameacha alama ya uongozi bora kutokana na malezi ya kitaaluma, msimamo
wake katika kusimamia maadili na weledi kazini, pamoja na juhudi zake za
kuwajengea uwezo Watumishi.
Alibainisha
kuwa uongozi wake umeweka msingi imara wa uwajibikaji, uadilifu na heshima
katika mazingira ya kazi, hali iliyochangia kuimarika kwa utendaji wa Mahakama Geita.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa Viongozi na Watumishi mbalimbali kutoa salamu za shukrani na pongezi kwa Mhe. Mhina kwa mchango wake katika maendeleo ya Mahakama Geita, huku wakimtakia mafanikio zaidi katika majukumu yake mapya.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina, akitoa shukurani.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akimulishakeki Jaji wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Griffin Mwakapeje.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna Pamoja na Mtendaji wa Mahakama Geita,
Bi. Masalu Kisasila.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama
Kuu Geita.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Geita.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa katika picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya wilaya Geita.
Picha Namba 7. Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama
ya Wilaya Chato.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bukombe.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Nyanghwale.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Biashara, Mhe. Kevin
Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbogwe.










Hakuna maoni:
Chapisha Maoni