Jumanne, 16 Juni 2026

USHIRIKIANO KAZINI NI NYENZO MUHIMU KATIKA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga amesema ushirikiano na mahusiano mazuri kazini ni nyenzo muhimu katika kuboresha utendaji kazi ujumbe huo ameutoa wakati alipotembelea Mahakama zilizopo Mbeya Mjini ikiwa ni kuanza kwa ukaguzi wa kawaida warobo ya nne ya mwaka 2025/2026.

Ziara hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Juni, kwa kutembelea sehemu ya Mahakama kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Mahakama hizo na alipata wasaa wa kuzungumza na watumishi wa Mahakama hizo katika vikao vya pamoja vilivyofanywa wakati wa ziara hiyo.

Akizungumza katika vikao hivyo, vilivyofanyika katika ukaguzi huo, Mhe. Tiganga alisisitiza kudumisha nidhamu, ushirikiano na mahusiano mazuri mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa watumishi katika kupanga mambo mbalimbali ya kiutendaji.

“Nasisitiza kudumisha nidhamu na mahusiano mazuri kazini, tuishi kwa upendo na tujifunze kuvumiliana pale inapotokea kupishana baina yetu, tuepuke mambo ambayo hayana ulazima Kutugawa, tusitengeneze ugumu wa kazi kwa kuwekeana vinyongo na vikwazo baina yetu. Pia nawakumbusha kuhusu umuhimu wa ushirikishwaji wa watumishi katika kupanga mambo mbalimbali ya kiutendaji katika ofisi zetu,” alisema Mhe. Tiganga katika ziara yake hiyo.

Mhe. Tiganga aliongezea kwa kusisitiza umuhimu wa kutunza na kulinda rasilimali za Mahakama na kuzingatia hasa vipaumbele vya ofisi kulingana na bajeti zenu kila fedha za matumizi ya ndani zinapoletwa.

Aidha Mahakimu Wafawidhi wa Vituo hivyo alivyotembelea walitoa shukrani zao kwa ziara hiyo na kuahidi kuwa wako tayari kutekeleza yale yote waliyoelekezwa na viongozi wao ili kuboresha utendaji kazi katika vituo vyao na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, kupitia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa na Mahakimu Wafawidhi wa Vituo mbalimbali alivyotembelea zilieleza juu ya usimamizi wa rasilimali mbalimbali zilizopo, utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na hali ya mashauri katika vituo hivyo.

Sambamba na hilo, Taarifa hizo zilieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika vituo vyao ambapo wengi wao walieleza hasa kuhusu uhaba wa watumishi hasa kada ya walinzi, uchakavu wa vyombo vya usafiri na uchakavu wa majengo hasa kwa Mahakama za mwanzo.

Katika ziara hiyo Mhe. Tiganga, aliambatana na viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, akiwemo Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo, Afisa Utumishi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bw. Moses Luoga na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Watoto Mbeya.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akiwa ndani ya Ofisi ya Mahakama ya hakimu mkazi Mbeya, kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Majala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo na kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati walioketi mbele). akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, walioketi mbele, kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti na kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya wilaya Mbeya katika ukaguzi huo, wanne kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya, Mhe. Tedy Mlimba.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (katikati) akizungumza jambo kwenye moja ya vikao katika ziara hiyo.

Sehemu ya Watumishi wakimsikiliza Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (hayupo pichani) akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa mbele)akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa mbele)akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni