Ijumaa, 26 Juni 2026

WATUMISHI MBEYA WAWAAGA VIONGOZI WAO

Na. MUKSINI NAKUVAMBA - Mahakama, Mbeya.

Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya waliandaa hafla maalumu ya kuwaaga viongozi wao waliowahi kufanya kazi nao kwa karibu, wakielezea shukrani zao kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuimarisha utendaji kazi, ustawi wa watumishi na maendeleo ya Taasisi.

Hafla hiyo iliyofanyika katika viunga vya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya iliwakutanisha viongozi na watumishi mbalimbali katika mazingira yaliyojaa hisia za furaha na huzuni kwa wakati mmoja.

Aidha, furaha ilitokana na kuwatakia viongozi hao kila la heri na mafanikio katika majukumu yao mapya, huku huzuni ikitokana na kuondoka kwa viongozi ambao walijijengea heshima na upendo mkubwa miongoni mwa watumishi kutokana na uongozi wao wenye busara, ushirikiano na kujali maslahi ya watumishi.

Viongozi walioagwa ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Emily Temu, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Timoth Lyimo na Mtendaji wa Mahakama kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bi. Mavis Fransis Miti, ambao kwa nyakati tofauti walipokea pongezi na maneno ya shukrani kutoka kwa watumishi waliopata fursa ya kufanya kazi chini ya uongozi wao.

Kwa upande wao, viongozi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya pamoja na watumishi waliopata nafasi ya kuzungumza walieleza kuwa viongozi hao wameacha alama kubwa katika taasisi kutokana na uadilifu, uwajibikaji na moyo wa kujali watu waliouonesha katika kipindi chote cha utumishi wao.

Miongoni mwa shughuli zilizofanyika katika hafla hiyo ni utoaji wa maneno ya shukrani kwa waagwa, utoaji wa zawadi maalum kama ishara ya kuthamini mchango wao, kukata keki pamoja na kula chakula cha pamoja, matukio yaliyoongeza mshikamano na kuacha kumbukumbu ya pekee kwa washiriki wote.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa dua na salamu za heri, ambapo watumishi walisisitiza kuwa milango ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya itaendelea kuwa wazi kwa viongozi hao na kwamba mchango wao utaendelea kukumbukwa kwa muda mrefu kutokana na athari chanya waliyoiacha katika taasisi na kwa watumishi kwa ujumla.

Waagwa wakiwa kwenye picha ya Pamoja katika hafla hiyo kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu, (katikati) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bi. Mavis Fransis Miti na kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Timoth Lyimo

Viongozi waagwa katika hafla hiyo wakikata keki kwa Pamoja ikiwa ni Ishara ya upendo na mshikamano

Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Timoth Lyimo akitoa neno wakati wa hafla ya kuagwa.

Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Said Kalunde (kushoto) akitoa nasaa kwa Viongozi Waagwa.

Sehemu ya watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya walioshiriki kwenye hafla hiyo.

Sehemu ya watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya wakiwa wamebeba zawadi zilizoandaliwa kwa ajili ya Viongozi wanaoagwa (hawapo pichani).

Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu akitoa neno la shukurani katika hafla hiyo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bi. Mavis Fransis Miti akitoa neno la shukurani katika hafla hiyo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akizungumza katika hafla hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Paul Dandi Ntumo akitoa neno la shukurani katika hafla hiyo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akikabidhi Zawadi kwa Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Timoth Lyimo.

Viongozi wa Mahakama Kuu masjala Ndogo ya Mbeya kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Mussa Pomo, Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Said Kalunde (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Fahamu Mtulya (wa pili kulia) na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Angaza Mwipopo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe, Fahamu Mtulya akimlisha keki Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bi. Mavis Fransis Miti.






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni