Jumatano, 29 Julai 2026

MAHAKAMA KUU DODOMA YAWAKARIBISHA MAJAJI NA WATUMISHI WALIOHAMISHIWA KITUO HICHO; YAWAAGA WALIOHAMA

Na ARAPHA RUSHEKE, Mahakama-Dodoma

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dodoma imefanya hafla ya kuwakaribisha Majaji pamoja na Watumishi waliohamia katika Mahakama hiyo na kuwaaga waliohamishwa kutoka Mahakama hiyo.

Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa 'Royal Village' jijini Dodoma na kuwakutanisha Majaji, Wasajili, Viongozi na Watumishi wa Mahakama kutoka katika Vituo mbalimbali vya Mahakama Dodoma ililenga kuwaaga watumishi waliopata uhamisho pamoja na kuwakaribisha wale waliopangiwa kuanza majukumu katika Mahakama hiyo.

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria hafla hiyo walikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Juliana Masabo ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma aliagwa kufuatiwa kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Rufani, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga aliyekaribishwa baada ya kuhamia Dodoma kuwa Mfawidhi wa Masjala hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara,  Mhe. Evarist  Longopa ambaye aliagwa baada ya kuhamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara Dar es Salaam. 

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni Majaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Biswalo Mganga, Mhe. Suleiman Hassan, Mhe. Irene Musokwa pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama hiyo.

Kulikuwa pia na Watumishi wa kada mbalimbali ambao wameagwa na kukaribishwa, watumishi hao ni pamoja na wa Kada za Watunza kumbukumbu, Wasaidizi wa Ofisi, Madereva, Mwandishi Mwendesha Ofisi pamoja na Wasaidizi wa Sheria.

Shughuli za hafla zilianza kwa kuwasili kwa wageni waalikwa na wageni rasmi, zikafuatiwa na dua fupi, utambulisho wa wageni, kukata keki na shughuli mbalimbali za kijamii zilizolenga kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa Mahakama pamoja na wadau .

Aidha, wageni walipata fursa ya kutoa salamu za pongezi na shukrani, kutoa zawadi kwa wahusika pamoja na kusikiliza nasaha na hotuba zilizosisitiza umuhimu wa kudumisha maadili, uwajibikaji na ushirikiano katika utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.

Hafla hiyo ilipambwa na shamrashamra pamoja na muziki kutoka Bendi ya Magereza Dodoma ambao ni Wadau wakubwa wa Mahakama.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa kupata chakula cha pamoja na burudani ya muziki, ambapo washiriki walipata nafasi ya kuendelea kujenga mahusiano mema na kuimarisha umoja ndani ya familia ya Mahakama.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt Juliana Masabo (kulia) akisikiliza kwa makini ujumbe wa zawadi yake kutoka kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma ambayo iliwasilishwa kwake na Jaji Mfawidhi  wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Joachim Tiganga wakati wa sherehe ya kuwaaga na kuwakaribisha Watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma iliyofanyika katika ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.


    Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe.Dkt Juliana Masabo wa kwanza kulia akisikiliza kwa makini ujumbe wa zawadi yake kutoka kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma ambayo iliwasilishwa kwake na Jaji Mfawidhi  wa Mahakama Kuu Dodoma Mhe Joachim Tiganga wakati wa sherehe hiyo.


Jaji Mfawidhi  wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masajala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (kulia) akipokea  dhawadi yake kutoka kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma iliyowasilishwa kwake na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Biswalo Mganga wakati wa sherehe hiyo.


 
 Matukio katika picha Sherehe ya Kuwakaribisha watumishi waliohamia Mahakama Kuu na kuwaaga Watumishi waliohama kutoka Mahakama hiyo.



(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni