Na MARY GWERA, Mahakama - Dodoma
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 25 Julai, 2026 ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Jacob John Mkunda, Viongozi wa Serikali na Watanzania wote kwa ujumla kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini.
Hafla ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini imefanyika katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Mji wa
Serikali-Mtumba jijini Dodoma huku ikitawaliwa na ratiba mbalimbali ikiwemo
utoaji wa dua na sala.
Katika maadhimisho hayo, Viongozi mbalimbali pia walishiriki kutoa heshima kwa kuweka vifaa na alama za jadi kwenye Mnara wa Mashujaa wakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka Mkuki na Ngao kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwaenzi, kuwakumbuka na kuthamini mchango wa mashujaa waliopigania uhuru, amani na maendeleo ya Taifa.
Kadhalika Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda aliweka Sime; Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana aliweka shada la maua kwa niaba ya Mabalozi, Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula aliweka Upinde na Mshale huku Brigedia Jenerali (Mstaafu), Wilfred Paul Mwakalambile Kabunda akiweka Shoka.
Mbali na Jaji Mkuu, Viongozi wengine waliohudhuria katika Sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na wengine.
Aidha kwa upande wa
Mahakama, sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Sam Rumanyika, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Dkt. John Antony Jingu, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Chiganga
Tengwa na baadhi ya Viongozi wengine.
Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania huadhimishwa tarehe 25 Julai kila mwaka lengo likiwa ni kuwakumbuka na kuwaenzi Mashujaa wote waliopoteza maisha yao wakitetea, kupigania na kulinda uhuru, amani, umoja na maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo yanaendelea kuwa chachu ya kuhamasisha uzalendo, mshikamano na uwajibikaji kwa vizazi vya sasa na vijavyo katika kulijenga Taifa la Tanzania.

Matukio katika picha Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Nchini leo tarehe 25 Julai, 2026 katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.Picha mbalimbali za matukio ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa nchini leo tarehe 25 Julai, 2026 katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Burudani ikiendelea.
Mnara wa Mashujaa.






















Hakuna maoni:
Chapisha Maoni