- Atoa mada kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wapya
Jaji Mstaafu wa Mahakama
ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa jana tarehe 09 Julai, 2026 alimtembelea Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju na kupata fursa ya kufanya naye mazungumzo mafupi ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Aidha, kabla ya kumtembelea Jaji Mkuu, Mhe. Rutakangwa alitoa mada tatu kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wapya tisa wanaopatiwa Mafunzo Elekezi kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa kuanza
kutekeleza majukumu yao katika ngazi hiyo ya juu katika mfumo wa utoaji haki
nchini.
Mada alizotoa kwa Majaji hao ni Sheria ya
Mahakama ya Rufani (Appellate Jurisdiction Act) pamoja na Kanuni za Uendeshaji
Mashauri katika Mahakama ya Rufani (Court of Appeal Rules, Madaraka ya Mahakama
ya Rufani kurejea maamuzi (Suo Motto Revisional Powers of the Court of Appeal)
pamoja na Maombi ya Marejeo (Application for Revision).
Mhe. Rutakangwa leo tarehe 10
Julai, 2026 anawapitisha Majaji hao wapya wa Mahakama ya
Rufani katika mada inayohusu Maombi ya Mapitio (Application for Review) na
mwisho eneo la ufanyaji kazi wa pamoja (Collegiality at the Court of Appeal).
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa wakati Jaji Mstaafu, Mhe. Rutakangwa alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 09 Julai, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa wakiwa katika wakizungumza jambo wakati Jaji Mstaafu, Mhe. Rutakangwa alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 09 Julai, 2026.
Picha ya pamoja, kulia ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akiwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa wakati Jaji Mstaafu, Mhe. Rutakangwa alipomtembelea na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 09 Julai, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa wakati Jaji Mstaafu huyo alipomtembelea na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 09 Julai, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyesimama mbele kushoto) akizungumza na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Edward Rutakangwa wakati Jaji Mstaafu huyo alipotoa mada kwa Majaji wapya wa mahakama ya Rufani tarehe 09 Julai, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni