Jumatano, 15 Julai 2026

KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA AJITAMBULISHA RASMI KWA JAJI MKUU

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, leo tarehe 15 Julai, 2026 amepokea ugeni wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe, aliyefika ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha.

Dkt. Shekalaghe amesema kuwa lengo la kukutana na Jaji Mkuu ni kujitambulisha rasmi kwake, kufuatia kuteuliwa kwake hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika nafasi hiyo. 

"Mhe. Jaji Mkuu, nimefika kujitambulisha kwako rasmi kwa nafasi yako kama Kiongozi Mkuu katika Mhimili huu wa Mahakama. Lakini pia kama kuna lolote niweze kupokea maelekezo. Ndilo lengo hasa kubwa kwa nini nimefika hapa," ameeleza Katibu Mkuu huyo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe (aliyesimama) akijitambulisha mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 15 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji
 
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe aliyemtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 15 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe (wa kwanza kulia kwa Jaji Mkuu) wakati alipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 15 Julai, 2026 kwa lengo la kujitambulia. Wa kwanza kushoto kwa Jaji Mkuu ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu, kushoto kwa Jaji Kiongozi ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, anayefuatia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Venance Mlingi, anayefuatia ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Mussa Hamza .

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (katikati) na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Venance Mlingi wakifuatilia mazungumzo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 15 Julai, 2026.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimuonesha Dkt. Shekalaghe (katikati) picha za ukutani za Majaji Wakuu waliopita (hawapo katika picha) wakati Katibu Mkuu huyo alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe  alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 15 Julai, 2026.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (wa pili kulia), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya na wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimuaga Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe mara baada ya kujitambulisha kwa Jaji Mkuu leo tarehe 15 Julai, 2026. 
















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni