Na SHARIFU MOKIWA-Mahakama, Sumbawanga
Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania wamewasili mkoani Rukwa kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya rufaa katika Kikao cha Mahakama ya Rufani kinachotarajiwa kufanyika katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Sumbawanga kuanzia tarehe 3 hadi 28 Agosti 2026.
Majaji hao wanaotarajiwa kuendesha vikao hivyo ni pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Ferdinand Leons Katipwa Wambali, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Lucia Gamuya Kairo na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Mustapha Ismail ambao wamewasili Sumbawanga kwa ajili ya kazi hiyo.
Majaji hao wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania walipokelewa mjini Sumbawanga na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga, Mhe. Pamela Mazengo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga, Bw. Machumu Essaba pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu Sumbawanga.
Kikao hicho kinatarajiwa kusikiliza jumla ya mashauri 38 ya jinai na madai, ambayo yanatoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Sumbawanga, Katavi, Mbeya, Mpanda na Songea, huku usikilizwaji wake ukifanyika katika Mahakama Kuu ya Masjala Ndogo ya Sumbawanga.
Akizungumzia kuhusu kikao hicho, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga, Mhe. Pamela Mazengo alisema kuwa, matarajio ya Mahakama ni kuhakikisha mashauri yote yaliyopangwa yanasikilizwa na kumalizika ndani ya kipindi cha kikao hicho kama ilivyopangwa.
“Matarajio yetu ni mashauri yote yaliyopangwa kusikilizwa na kumalizika, kwa kuwa hatua hii itawawezesha wahusika kutambua hatima ya mashauri yao na pia kupunguza mashauri yanayosubiri kusikilizwa,” alisema Mhe. Mazengo.
Aidha, Mhe.
Mazengo alisema kuwa, kufanyika kwa kikao hicho Sumbawanga ni
sehemu ya jitihada za Mahakama ya Tanzania kuboresha
huduma za kimahakama kwa kuwafikishia wananchi huduma hizo kwa urahisi zaidi,
pamoja na kupunguza mzigo wa mashauri yanayosubiri kusikilizwa.
Mapokezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwasili Uwanja wa Ndege (wa kwanza kulia) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Ferdinand Leons Katipwa Wambali, (wa pili kulia) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda, (wa pili kushoto) ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga, Mhe. Pamela Mazengo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Mhe. Wanje Hamza (wa kwanza kulia) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Lucia Kairo, (aliyevalia kitenge) walipopokelewa baada ya kuwasili mjini Sumbawanga.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Lucia Kairo (kushoto) akisalimiana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Lillian Ndelwa.
Viongiozi wa Mahakama ya Tanzania Masjala Ndogo ya Sumbawanga
wakisalimiana na Jaji wa Mahakama ya Rufani mara walipowasili mjini Sumbawanga,
(Kulia) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Ferdinand
Leons Katipwa Wambali, akisalimiana na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo
ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba, na (katikati) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya
Tanzania, Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda.
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni