Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama Mbeya
Watumishi
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya jana tarehe 15 Julai, 2026 walishiriki
katika hafla ya kumuaga aliyekuwa mtumishi Mahakama mstaafu Bw. Charles Mapunda
Chiteketela, ambaye alikuwa akihudumu kama Msaidizi wa Kumbukumbu na Msimamizi
wa Kitengo cha mashauri ya Madai, anayestaafu utumishi wa umma baada ya
kuitumikia Mahakama kwa weledi, uadilifu na kujituma kwa muda wa miongo kadhaa.
Hafla
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Mbeya na kuhudhuriwa na Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Benard Mpepo,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mbeya, Mhe. Teddy Mlimba, viongozi
mbalimbali wa vitengo pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Wilaya
Mbeya.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mpepo alimpongeza Bw. Mapunda kwa utumishi wake
uliotukuka na mchango mkubwa alioutoa katika kuimarisha utendaji wa Mahakama.
Alieleza kuwa mstaafu huyo amekuwa mfano wa uwajibikaji, uaminifu na uzalendo
katika kutekeleza majukumu yake.
“Tunakupongeza
sana Bw. Mapunda, umekuwa mtumishi uliyeitumikia Mahakama kwa utumishi
uliotukuka. Tunazijua na kuzithamini kazi ulizozifanya na kwa juhudi zako
uliendelea kujiendeleza hadi kufika hapo ulipo, kwa hakika uliipenda na
kuiheshimu kazi yako Mungu akubariki katika maisha yako mapya,” alisema Mhe.
Mpepo.
Kwa
upande wake, mstaafu huyo Bw. Chiteketela alitoa shukrani kwa viongozi na
watumishi wote aliobahatika kufanya nao kazi kwa kipindi chote cha utumishi
wake. Alisema ushirikiano, upendo na mshikamano alioupata kutoka kwa wenzake
umechangia mafanikio yake katika kazi.
“Napenda
kuwashukuru watumishi wenzangu ambao tumefanya kazi pamoja kwa ushirikiano
mkubwa bila kuchoka na bila kubaguana. Nawashukuru pia viongozi wangu kwa
kunilea na kuniongoza vyema hadi kufikia hatua hii, Mungu awabariki sana.”
Aidha, Bw.
Chiteketela aliwaasa watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi,
bidii na uaminifu, akisisitiza kuwa mafanikio katika utumishi yanatokana na kuipenda
kazi na kutimiza wajibu kwa moyo wa kujituma.
“Ukifanya
kazi kwa weledi na kujituma haikupi shida kuifanikisha kazi yako. Nawausia
kuipenda kazi yenu na kujituma katika majukumu yote mnayopangiwa na viongozi,
kwani huo ndiyo msingi wa mafanikio,” alisisitiza Bw. Chiteketela
Bw.
Mapunda aliwahimiza watumishi kudumisha umoja na ushirikiano mahali pa kazi ili
kuendelea kujenga mazingira bora ya utendaji na kuimarisha mahusiano ya kikazi.
“Nawasihi
muwe na umoja na ushirikiano baina yenu, kwa kuwa kufanya hivyo kutaboresha
utendaji kazi na kujenga undugu imara baina yenu.”
Hafla
hiyo imeendelea kudhihirisha utamaduni wa Mahakama wa kuthamini na kuenzi
mchango wa watumishi wake waliotumikia taasisi kwa uaminifu, uadilifu na
kujituma.
Mtumishi
Mstaafu Bw.
Charles Mapunda Chiteketela (kulia) akizungumza machache na kutoa
neno la shukurani katika hafla hiyo.
Bw.
Charles Mapunda Chiteketela (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na
Mahakimu Mbalimbali wakiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
Mbeya, Mhe. Teddy Mlimba (watatu kushoto)
Bw.
Charles Mapunda Chiteketela (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi
ya watumishi wa kitengo cha madai ambacho Bw. Charles Mapunda Chiteketela
alikuwa msimamizi wa kitengo hicho
Bw.
Charles Mapunda Chiteketela (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na
maafisa Utumishi/Tawala (wa kwanza kushoto) ni Afisa Utumishi Mahakama ya
Watoto Mbeya Bw. Ibrahim Mgallah, (wa pili kushoto) ni Afisa Utumishi Mahakama ya
Wilaya Mbeya Bi. Odilia Mapunda, (wa kwanza kulia) ni Afisa Utumishi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya
Mbeya Bi. Sarah Lossi a aliyesimamama nyuma ni Afisa Utumishi Mahakama Kuu
Masjala ndogo ya Mbeya Bw. Alintula Ngalile.
Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Benard Mpepo (kushoto) akikabidhi sehemu ya zawadi zilizoandaliwa kwa Mtumishi Mstaafu Bw. Charles Mapunda Chiteketela (kulia) wakati wa hafla hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni