Jumanne, 11 Agosti 2026

JAJI KIONGOZI AKAGUA JENGO LINALOTARAJIWA KUWA MAHAKAMA YA FAMILIA DODOMA

Na ARAPHA RUSHEKE -Mahakama, Dodoma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, jana tarehe 10 Agosti, 2026, alifanya ziara katika jengo la zamani la Mahakama Kuu Dodoma, linalotarajiwa kutumika kwa ajili ya Mahakama inayoshughulikia masuala ya familia.

Akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Mahakama, Jaji Kiongozi alikagua miundombinu ya jengo hilo na kujionea maboresho yanayoendelea kufanyika.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Siyani aitoa maelekezo mbalimbali yanayolenga kusaidia katika uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya jengo hilo, ili liweze kuwa na mazingira bora kwa ajili ya utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Mahakama katika kuhakikisha miundombinu yake inaendelea kuboreshwa, sambamba na kuimarisha mazingira ya utoaji wa huduma za haki.

PICHA CHINI ZINAOONESHA ZIARA HIYO

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akiendelea na ukaguzi mara baada ya kuwasilia katika jengo la zamani la Mahakama Kuu Dodooma, ambalo linatarajiwa kuwa Mahakama ya Familia Dodoma.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akiangalia sehemu ya mapokezi ya jengo hilo ambalo linatarajiwa kuwa Mahakama ya Familia Dodoma.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akisikiliza maelezo ambayo yalikuwa yanatolewa na moja ya wakandarasi waliokuwa katika jengo hilo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akiendelea na ukaguzi.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akikagua mazingira ya nje ya jengo hilo(juu na chini).


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akiwaelekeza jambo wakandarasi wakati wa ukaguzi huo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akizungumza na Viongozi alioambatana nao katika ukaguzi huo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akijadili jambo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya.

Habari hii imehririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni