Jumatano, 12 Agosti 2026

MAHAKAMA, TUME YA MIPANGO KUSHIRIKIANA UTEKELEZAJI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na baadhi ya Viongozi wengine wa Mhimili huo leo tarehe 12 Agosti, 2026 wametembelewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida pamoja na baadhi ya Viongozi wengine wa Tume hiyo kwa lengo la kufanya mazungumzo na Mahakama ya Tanzania ili kujadiliana kuhusu namna Taasisi  hizo mbili zitakavyoshirikiana katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050.

Dkt. Kida amesema, Mahakama ya Tanzania ina mchango mkubwa katika utekelezaji wa Dira hiyo.

Aidha, Dkt. Jingu amesema Mahakama ya Tanzania imeshaanza utekelezaji wa Dira hiyo na ipo tayari kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Matukio katika picha mazungumzo kati ya Mahakama ya Tanzania na Tume ya Taifa ya Mipango.


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida (katikati) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (kushoto) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya leo tarehe 12 Agosti 2026 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida akisaini  kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu leo tarehe 12 Agosti, 2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Sehemu ya Viongozi wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania na Viongozi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango wakiwa katika kikao cha majadiliano juu ya ushirikiano katika ya Ofisi hizo katika utekelezaji wa pamoja wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050 leo tarehe tarehe 12 Agosti, 2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Anyeongoza kikao hicho (aliyeketi mbele katikati) ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu, kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida na kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya.


Mazungumzo kati ya Viongozi wa Mahakama ya Tanzania na Tume ya Taifa ya Mipango yakiendelea leo tarehe 12 Agosti, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (katikati) akipokea Nyenzo ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida leo tarehe 12 Agosti 2026 jijini Dodoma katika kikao kati ya Mahakama ya Tanzania na Tume ya Mipango kilicholenga kujadiliana kuhusu namna Mahakama itakavyoshirikiana na Tume hiyo katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu akimpatia Nyenzo za Utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida (kulia) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya.

(Picha na HALIMA MNETE, Mahakama)







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni