Na IMAN MZUMBWE - Mahakama, Songwe
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Songwe imeanzisha programu maalum ya mazoezi
ya viungo ili kujenga utimamu wa mwili ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
kujiandaa na mashindano mbalimbali, kuimarisha afya na kuongeza mshikamano
miongoni mwa watumishi wa Mahakama. Programu hayo ya mazoezi itakuwa inafanyika
katika viunga vya Mahakama Kuu iliyopo Nselewa-Mlowo.
Programu
hiyo ya mazoezi inafanyika kwa kuwashirikisha watumishi mbalimbali wa Mahakama na
wadau ambao wanapata nafasi ya kufanya mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali
chini ya usimamizi wa viongozi wa michezo ambao ni Afisa michezo Bi. Collether
Amos Carlos, Mwenyikiti wa michezo Bw. Iman Patson na Katibu wa michezo Bi. Joyce
Simba.
Akizungumza
wakati wa kuanza mazoezi hayo, Afisa Michezo Bi. Collether Amos Carlos, amewaasa
na kuwahimiza watumishi kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu katika
mazoezi hayo na akisisitiza kuwa, michezo ni muhimu katika kuimarisha afya,
kujenga umoja, ushirikiano na kuongeza morali ya utendaji kazi.
Aidha,
Bi. Collether ameongeza kuwa, mazoezi hayo yataendelea kwa utaratibu maalum ili
kuhakikisha watumishi wanakuwa katika hali nzuri kiafya na kuwa tayari
kushiriki katika mashindano mbalimbali yatayokutanisha watumishi wa Mahakama na
wadau wengine, huku Kaulimbiu ya programu hiyo ikiwa ni; “Afya bora, umoja na ushiriakiano
kwa utendaji bora wa kazi”.
Afisa
Michezo Bi. Collether Amos Carlos wa (kwanza kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na watumishi wa Mahakama Songwe.
Mwalimu
wa michezo Bw. Martin Pales Kambengwa akitoa mazoezi mbele ya watumishi wa Mahakama
ambao hawapo katika picha.
Watumishi
wa Mahakama wakifanya mazoezi ya kucheza mpira wa mikono yaani netball
Watumishi
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Songwe wakifanaya mazoezi mepesi (warm up)
Watumishi
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Songwe wakifanaya mazoezi mepesi ya kupasha misuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni