Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Uongozi
na Watumishi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya wameendeleza dhamira yao
ya dhati ya kujenga afya bora ya mwili na akili kupitia programu ya mazoezi ya
pamoja inayofanyika kila Jumanne na Ijumaa ya kila wiki katika viunga vya
Mahakama Kuu Masjala hiyo.
Mazoezi
hayo yanawakutanisha viongozi, wadau na watumishi wa kada mbalimbali katika
mazingira yanayosaidia kukuza mshikamano, ushirikiano na ustawi wa afya, ikiwa
ni sehemu ya kuhamasisha utamaduni wa kujali afya mahali pa kazi.
Ushiriki
wa Viongozi na Watumishi hao umeendelea kuwa chachu ya kuwahamasisha watumishi wengine
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, jambo linalosisitiza kwamba, uwepo wa
afya njema ni msingi muhimu wa kuongeza ufanisi, tija na ubora wa utoaji huduma
za haki kwa wananchi.
Mbali
na kuimarisha afya ya mwili, mazoezi hayo yamekuwa yakisaidia kupunguza msongo
wa mawazo, kuongeza nguvu ya kiutendaji na kuimarisha mahusiano ya kikazi
miongoni mwa watumishi wa Mahakama.
Nayo, timu ya mpira wa miguu ya Mahakama “Mbeya Mahakama
sports” inayoundwa na wachezaji kutoka Mahakama zilizopo Mbeya Mjini imeendelea
kufanya mazoezi yake katika viwanja mbalimbali huku ikiwa na mwendelezo mzuri wa
kupata matokeo uwanjani.
Timu hiyo hivi karibuni imecheza mechi za kirafiki na
baadhi ya timu za mpira wa miguu za taasisi na timu za wanachi huku wakiibuka
na ushindi kwa mechi tatu mfululizo na kupata sare kwa mechi moja pekee
iliyochezwa hivi karibuni na timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa Hospitali
ya Mkoa wa Mbeya.
Mwamko
huo wa kufanya mazoezi kwa watumishi unaendelea kujenga taswira inayotambua
kuwa mtumishi mwenye afya bora ni nguzo muhimu katika utoaji wa haki kwa wakati
na kwa ubora unaostahili.
Aidha,
kupitia utaratibu huo wa mazoezi ya kila wiki, Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya inaendelea kuonesha mfano kwamba uwekezaji katika afya ya watumishi ni
uwekezaji katika huduma bora kwa wananchi. Vilevile ushiriki wa pamoja kati ya
watumishi wa Mahakama na wananchi katika michezo mbalimbali ni chachu ya
kuisaidia Mahakama kuongeza imani ya Mahakama kwa wananchi.
Sehemu ya viongozi, wadau na watumishi Mahakama wa Kada mbalimbali wakiwa kwenye mazoezi ya pamoja yaliyowakutanisha kwa ajili ya kujenga afya ya mwili na akili ili kurejesha utimamu wa mwili katika mahala pa kazi, mazoezi hayo yanafanyika katika viunga vya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.
Sehemu ya matukio katika mazoezi mbalimbali
yanayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya apo.
Sehemu ya matukio katika mazoezi mbalimbali yanayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya apo.
Sehemu ya matukio katika mazoezi mbalimbali
yanayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya apo.
Timu
ya mpira wa miguu ya Mahakama Kuu Mbeya ikiendelea na mazoezi yake katika
uwanja cha shule ya msingi Nzovwe Mbeya kujiandaa na mechi zinazoendelea za
kirafiki.
Jaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (kushoto) akiwa katika
mazoezi pamoja na sehemu ya watumishi alioshiriki na mazoezi hayo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (Kushoto) na Mtendaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo Chonya (kulia) wakiendelea
kufanya mazoezi katika viunga vya Mahakama Kuu jijini Mbeya.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (wa kwanza
kulia) akizungumza machache wakati wa kufunga mazoezi. (wa kwanza kushoto) ni Jaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo na Mtendaji wa Mahakama
Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo Chonya (wanne kulia)
Sehemu ya Viongozi wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya wakiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu
Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (watano kutoka kushoto) akiwa kwenye picha
ya pamoja na sehemu ya watumishi wa kada mbalimbali baada ya mazoezi ya pamoja
katika viunga vya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
.jpeg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni