Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu leo tarehe 18 Agosti, 2026 amefanya ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania - Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
Dkt. Jingu ametembelea Mahakama hiyo kwa lengo la kuzungumza na watumishi pamoja na kujua hoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Aidha, Mtendaji Mkuu amewasikiliza Watumishi hao na kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na nyingine ameahidi kuzishughulikia.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi alipotembelea Mahakama hiyo leo tarehe 18 Agosti, 2026 Mikocheni B jijini Dar es Salaam. Aliyeketi kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Divisheni Maalum, Bi. Mary Shirima na kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Magdalena Ntandu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Sharmillah Sarwatt (kushoto) na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Dkt. Dafina Ndumbaro.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Sharmillah Sarwatt (wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Dkt. Dafina Ndumbaro (wa pili kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Divisheni Maalum, Bi. Mary Shirima (wa kwanza kushoto) na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Magdalena Ntandu.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni