Na CHRISTOPHER MSAGATI - Mahakama, Manyara
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Manyara iliwaalika watumishi kutoka Mahakama
Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora kwa ajili ya mafunzo na kubadilishana uzoefu wa
majukumu. Ziara hiyo imefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 17 na 18 Agosti,
2026 ili kuwapa watumishi hao fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya
kimahakama.
Aidha,
watumishi hao waliofika kutoka Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora ni Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Mhe. Rhoda Ngimilanga na Mtendaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Tabora Bw. Emmanuel Munda
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo ya kikazi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya
Manyara Mhe. Dkt. Adam Mambi aliwapongeza watumishi hao wa Tabora kwa kuichagua
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara kwa ajili ya mafunzo hayo na kuwaeleza
kuwa Manyara ni mahali sahihi pa kujifunza.
“Tunawakaribisha
Manyara, hapa ni mahala sahihi kwenu pa kujifunza. Tumekuwa tukiwawezesha hata
wanafunzi wa vyuo mbalimbali kupata mafunzo yao kwa ajili ya kutimiza vigezo na
matakwa yao ya kielimu hivyo nanyi tunawakaribisha ili mjifunze na sisi pia
tujifunze kutoka kwenu,” alisema Mhe. Dkt. Mambi.
Naye,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Mhe. Rhoda Ngimilanga
aliushukuru uongozi wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Manyara kwa mapokezi
mazuri ikiwa ni pamoja na kuwapa nafasi ya kujifunza masuala mbalimbali
yanayohusu majukumu ya kila siku ya mahakamani.
“Tumesikia
mambo mazuri ambayo Wanamanyara mnayafanya hivyo nasi tukaona ni vema tufike tujifunze
kutoka kwenu pamoja na kushiriki uzoefu wa Masjala zetu ili tuboreshe utendaji
kazi wetu wa kila siku”, alisema Mhe. Ngimilanga.
Pamoja
na kushiriki namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku, viongozi hao wa
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora waliweza kujifunza namna ya uandaaji bora
wa taarifa mbali mbali za kimashauri pamoja na zile za Kiutawala ambazo huwa
zinapaswa kuwasilishwa katika vikao mbalimbali. Katika hatua hiyo, viongozi hao
waliweza kushiriki Kikao cha pamoja na viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu,
Masjala ndogo ya Manyara ambacho hufanyika kila wiki kwa ajili ya kupeana
taarifa na maelekezo mbalimbali ya kikazi.
Akitoa
shukrani kwa uongozi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara, Mtendaji wa
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Bw. Emmanuel Munda aliwapongeza watumishi
wa Manyara pamoja na viongozi wao kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi hali
ambayo inawezesha mashauri yao kwenda kwa haraka jambo ambalo linapunguza
mlundikano wa mashauri.
“Kwa
kweli tumeona jitihada zenu Wanamanyara katika usikilizwaji wa mashauri ya kila
siku lakini pia katika usimamizi wa rasilimali zenu, tunaahidi kutumia elimu
hii tuliyoipata katika kuboresha utendaji kazi wetu tutakaporejea Tabora.
Pamoja
na kupata elimu na kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi, Viongozi wa
Mahakama hizo waliweka mikakati ya kuwa Masjala rafiki hata katika masuala ya
kijamii na viongozi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora waliweka ahadi ya
kuwakaribisha watumishi wa Manyara kwenda Tabora kwa ajili ya kujifunza.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara Mhe. Dkt. Adam Mambi
(aliyekaa mbele), pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama Kuu wakiwa katika
mazungumzo ndani ya Ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya
Manyara pamoja na wageni waliotoka Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora kwa
ajili ya mafunzo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Manyara Mhe. Dkt. Adam Mambi (aliyesimama wa nne kutoka upande wa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Manyara pamoja na wageni wao waliotoka Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Tabora.
Afisa
Tawala wa Mahakama Kuu Manyara, Bw. Christopher Msagati akiwasilisha mada
katika mafunzo waliyokuwa wanapatiwa viongozi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Tabora
katika Ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Manyara.
Mtendaji
wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Bw. Emmanuel Munda (kushoto), pamoja
na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Mhe. Rhoda Ngimilanga
wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama
Kuu Manyara.
Mtendaji
wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Mhe Bw. Emmanuel Munda (aliyesimama)
akichangia mada wakati wa kikao cha kutoa taarifa kilichoambatana na mafunzo
kwa viongozi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora. Aidha, katika Runinga
wanaoonekana ni washiriki wa kutoka Mahakama za Wilaya na za Mwanzo zilizopo
katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara wakishiriki kwa njia ya video.
Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora Mhe. Rhoda Ngimilanga
(aliyesimama) akichangia mada wakati wa kikao cha kutoa taarifa kilichoambatana
na mafunzo kwa viongozi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara Mhe. Dkt. Adam Mambi (kulia) akifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinatolewa
katika Kikao kilichoambatana na mafunzo kwa viongozi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo
ya Tabora katika Ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Manyara. Wengine ni Jaji wa
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Manyara Mhe. Devotha Kamuzora na (kushoto) ni
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Manyara Mhe. Charles Mnzava.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Kansha)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni