Jumatatu, 3 Agosti 2026

MTENDAJI MKUU MAHAKAMA ASHIRIKI MKUTANO WA MAZUNGUMZO MAALUM KUHUSU UTEKELEZAJI DIRA 2050

  • Apokea Nyenzo za Utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa niaba ya Jaji Mkuu
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu leo tarehe 03 Agosti, 2026 ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo na Viongozi wengine mbalimbali kushiriki katika Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi na Sekta ya Umma kuhusu Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050.

Katika Mkutano huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amezindua pia Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 na kukabidhi Ufunguo wa Mtazamo Mpya, unaoashiria mwanzo mpya wa ushirikiano wenye uwazi na uaminifu kati ya Serikali na Sekta Binafsi.

Aidha, Rais, Mhe. Dkt. Samia amewapatia Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 Viongozi kadhaa akiwemo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu ambaye alipokea kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta binafsi wamehudhuria katika mkutano huo muhimu.

Matukio katika picha Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi na Sekta ya Umma kuhusu Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050 na Uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimkabidhi Nyenzo za Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiwa katika Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi na Sekta ya Umma kuhusu Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050 na Uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 uliofanyika leo tarehe 03 Agosti, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Nyenzo za Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi na Sekta ya Umma kuhusu Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2050 na Uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 leo tarehe 03 Agosti, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi mfano wa Ufunguo kama ishara ya mtazamo mpya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (wa pili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malick Akil (wa kwanza kushoto), Rais wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bi. Angelina Ngalula (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara Zanzibar (ZNCC), Bw. Ali Amour (wa kwanza kulia) baada ya uzinduzi Nyenzo za Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Agosti, 2026.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni