Jumamosi, 22 Agosti 2026

TLS DODOMA YAIMARISHA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA

Na ARAPHA RUSHEKE -Mahakama Kuu Dodoma.

Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Dodoma Chapter, ukiongozwa Bi. Mary Munissi, tarehe 21 Agosti,2026 umemtembelea Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, katika ofisi yake iliyopo Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma.

Katika kikao hicho, pande hizo zimezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto zinazowakabili, pamoja na namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Mahakama na Wanasheria ili kuhakikisha huduma za utoaji haki kwa wananchi zinaendelea kutolewa kwa ufanisi na kwa wakati.

Kikao hicho pia kimekuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kitaaluma kwa lengo la kuboresha zaidi huduma za haki katika eneo la Dodoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, akisalimiana na wageni kutoka TLS Dodoma mara baada ya kuwasili katika ofisi yake kwa mazungumzo.


 

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Upendo Ngitiri (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho mara baada ya kuwasili kwa wageni hao.


 

Mwenyekiti wa TLS Dodoma, Bi Mary Munissi (wa kwanza kushoto) akimsikiliza kwa umakini kilichokuwa kinajiri.


 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (aliyepo katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa TLS Dodoma, Bi. Mary Munissi (aliyepo kulia kwake) na aliyepo kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa TLS Dodoma, Bw, Anselm Mwampoma.


 

Jaji Mfawidhi  wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Joachim Tiganga (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya uongozi wa TLS Dodoma mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni