Alhamisi, 6 Agosti 2026

WANA 'TMJA' TAWI LA NJOMBE WAKUTANA

Na ABDALLAH SALUM, Mahakama-Njombe 

Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe hivi karibuni kilikutana na kufanya kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Tawi hilo, Mhe. Dennis Mujwahuzwi kwa kujumuisha Wanachama kutoka katika Wilaya zote za Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Njombe lengo likiwa ni kujijengea uwezo katika masuala ya kisheria na kupitia Mpango Mkakati wa TMJA kwa mwaka 2026/2027.

Awali akifungua kikao hicho, Mlezi wa Tawi ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe, Mhe. Victoria Nongwa aliwapongeza Wanachama na Viongozi wa Tawi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujitolea kulijenga Tawi na kuwa na utaratibu wa kukutana kufanya mafunzo ya kujijengea uwezo katika majukumu ya utoaji haki.

“Nawapongeza sana Viongozi wetu wa Tawi pamoja na Wanachama wote kwa umoja wenu, Tawi hili ni letu mambo tunayopanga lazima tuyatekeleze kwa pamoja, tukifanya hivyo Tawi letu litazidi kuwa imara zaidi. Mmefanya vizuri sana kukutana kama hivi kwa ajili ya kupitisha Mpango Mkakati nitafurahi kama mtajenga utaratibu wa kukutana mara kwa mara kujijengea uwezo katika masuala mbalimbali ya kisheria,” alisema Mhe.Nongwa.

Kikao hicho kilitanguliwa na ushauri uliohusishwa na mada mbalimbali ikiwemo utoaji wa adhabu mbadala ambapo Naibu Msajili, Mhe. Joseph Luambano alisisitiza katika mashauri ya jinai, utekelezaji wa amri za Mahakama katika mashauri ya madai pamoja na namna bora ya kupokea ushahidi wa kielektroniki katika Mahakama za Mwanzo.  

Akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Tawi hilo, Mhe. Dennis Mujwahuzwi aliwapongeza Wanachama kwa kushiriki kikao hicho na kujadiliana masuala mbalimbali yanayolenga utoaji haki.

Naye Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Njombe, Obadia Bwegoge aliwasisitiza Washiriki kujenga utamaduni wa kufanya vikao hivyo mara kwa mara kwa kuwa vinawajenga katika shughuli zao kila siku pamoja na kupata muda wa kujumuika pamoja.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe ambaye pia ni Mlezi wa Wana Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe, Mhe. Victoria Nongwa (wa kwanza kushoto) pamoja na Viongozi wenzake wakiwa katika kikao cha Chama hicho kilichofanyika hivi karibuni. Wa kwanza kutoka kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe, Mhe. Obadia Bwegoge. Aliyeketi katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe, Mhe. Dennis Mujwahuzwi, wengine ni Makatibu wa Chama hicho, wa pili kushoto ni Mhe.Barnaba Mwangi na wa pili kulia ni Mhe. James Muhoni.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe, Mhe. Victoria Nongwa akizungumza hivi karibuni na Wana Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe (hawapo katika picha) wakati wa kikao hicho.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Njombe, Mhe. Obadia Bwegoge akisisitiza jambo kwa Wana Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe wakati wa kikao kilichofanyika hivi karibuni.

Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Njombe, Mhe. Joseph Luambano akisisitiza jambo kwa Wana Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe wakati wa kikao kilichofanyika hivi karibuni.

 Aliyesimama na walioketi  ni sehemu ya Wajumbe wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Tawi la Njombe ambao ni Mahakimu kutoka Mahakama zilizopo Njombe.

Kikao kikiendelea.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni