Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya, ameanza ziara
ya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Masjala hiyo kwa lengo la kutathmini
utendaji wa kazi ili kubaini mafanikio na changamoto katika utoaji wa huduma,
mazingira ya kazi na miundombinu ya Mahakama.
Ziara
hiyo iliyoanza tarehe 03 Septemba 2026 ni sehemu ya utekelezaji wa Mahakama kusogeza
huduma za haki karibu na wananchi, ambapo Mhe. Mtulya anatembelea Mahakama
zinazotoa huduma pamoja na maeneo ambayo kwa sasa hayatoi huduma kutokana na
sababu mbalimbali, ikiwemo uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa majengo ya
kutolea huduma na maeneo ambayo tayari yametengwa na Serikali za vijiji kwa
kushirikiana na wananchi kwa ajili ya uanzishwaji wa huduma za Mahakama.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Mtulya ametembelea Mahakama ya Wilaya ya Kyela pamoja na
Mahakama za Mwanzo Busale, Ndobo, Ikolo na Kyela Mjini, ambapo amekagua hali ya
utendaji, mazingira ya kazi na miundombinu ya Mahakama hizo.
Aidha,
Mhe. Mtulya ametembelea maeneo ya Lema, Ipande, Mwaya na Kajunjumele, ambayo
kwa sasa hayatoi huduma za Mahakama, huku baadhi ya maeneo hayo yakiwa na
viwanja vilivyotengwa na Serikali za Vijiji kwa kushirikiana na wananchi kwa
ajili ya ujenzi wa Mahakama.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mtulya ameeleza kuwa kutembelea maeneo yenye viwanja
vilivyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ni muhimu katika kuhakikisha
maeneo hayo yanalindwa na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
“Katika
kutekeleza mkakati wa Mahakama wa kusogeza huduma za Mahakama karibu na
wananchi, ndiyo maana sisi tumekuja kutekeleza ziara hii ili kufanikisha
mkakati huo,” amesema Mhe. Mtulya.
Katika
kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama yanalindwa,
Mhe. Mtulya amewaelekeza viongozi wa maeneo husika kufuatilia upatikanaji wa
hati za umiliki na kuweka alama za utambuzi katika kingo za viwanja hivyo ili
kuvilinda dhidi ya uvamizi na matumizi yasiyokusudiwa.
Vilevile,
amesisitiza umuhimu wa kutunza miundombinu ya Mahakama iliyopo na kuboresha
mazingira ya kazi, ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira, upandaji na utunzaji
wa miti na kuhakikisha majengo pamoja na maeneo ya Mahakama yanatunzwa
ipasavyo.
Katika
eneo la utoaji wa haki mapema ipasavyo, Mhe. Mtulya ameelekeza kuendelea kuweka
mkazo katika usikilizaji na utatuzi wa mashauri ya vipaumbele, hususan mashauri
ya mirathi na ndoa, ili kupunguza muda wa wananchi kusubiri haki na kuongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma za Mahakama.
Viongozi
wengine walioshiriki ziara hiyo ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo
ya Mbeya, Mhe. Benard Mpepo, pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo
ya Mbeya, Bw. Festo Chonya.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati)
akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ndobo. Viongozi wengine alioambatana nao (wanne kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu
Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo Chonya, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo (wanne kulia) na watatu kulia ni Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Kyela Mhe. Rosta Mofuga.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa katika
ukaguzi wa viwanja mbalimbali vya mahakama katika ziara hiyo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa katika
ukaguzi wa viwanja mbalimbali vya mahakama katika ziara hiyo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa katika
ukaguzi wa viwanja mbalimbali vya mahakama katika ziara hiyo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa katika
ukaguzi wa viwanja mbalimbali vya mahakama katika ziara hiyo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, akipokelewa
Mahakama na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Kyela.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Ipande katika uwanja wa
Mahakama uliotengwa na Serikali ya Kijiji cha Ipande, (wanne kulia) ni Afisa
Mtendaji wa Kata ya Ipande Bw. Lugano Mwabulanga na (watano kushoto) ni Afisa
Ugani Kata ya Ipande Bw. Hamadi Mussa Kassim.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Lema katika eneo wa lililotengwa na Serikali ya Kijiji cha Lema, wanne kulia ni Mwenyekiti
wa Kijiji cha Lema Bw. Charles Emily Mwakabulufu, wanne kushoto ni Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Lema Bi. Joice Mkumbwa Kaminyoge.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati)
akiongoza kikao cha pamoja na watumishi (hawapo pichani) wa Mahakama ya Wilaya
Kyela, kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo
Chonya na Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya na Viongozi
wengine alioambatana nao wakiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa Mahakama
ya Wilaya Kyela.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Kyela Mjini Mhe, Nassir Alfred Msafiri akiwasilisha taarifa, kwa Viongozi hao waliowasili katika ziara hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni