Jumatano, 23 Septemba 2026

JAJI MFAWIDHI MUSOMA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAHAKAMA, MAGEREZA

Na KANDANA LUCAS-Mahakama Kuu Musoma

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki, hivi karibuni alifanya ziara ya ukaguzi wa Mahakama zilizopo katika Kanda ya Musoma, pamoja na Magereza mbalimbali ya Wafungwa na Mahabusu mkoani Mara.

Akiongea na watumishi wa Mahakama alizokagua, Mhe. Kakolaki aliwapongeza kwa utendaji kazi mzuri, kwani Mahakama mbalimbali zilionekana kuwa na kiwango kizuri cha kasi ya umalizaji wa mashauri. 

Aidha, Jaji Kakolaki aliwasisitiza watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kusikiliza mashauri kwa wakati ili kuepuka mlundikano.

Vilevile alipotembelea Magereza, Jaji Kakolaki alisikiliza changamoto mbalimbali za Wafungwa na Mahabusu na kuzitolea ufafanuzi. 

Ukaguzi huo ni wa robo ya tatu ya mwaka 2026, ambapo jumla ya Mahakama za Wilaya sita na Mahakama za Mwanzo 13 zilikaguliwa, pamoja na Magereza matano ambayo ni Gereza la Wilaya Tarime, Gereza la Wafungwa na Mahabusu Mugumu, Gereza la Wilaya Bunda, Gereza la Kilimo na Mifugo Kiabakari na Gereza la Wilaya Musoma.

Viongozi wengine walioambatana na Jaji Mfawidhi katika ukaguzi huo ni Naibu Msajili, Mhe. Omari Kingwele na Mtendaji wa Mahakama, Bw. Leonard Maufi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki akiongea na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bunda (hawapo pichani). Wengine ni Naibu Msajili, Mhe. Omari Kingwele (kushoto) na Mtendaji wa Mahakama, Bw. Leonard Maufi (kulia).

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati  mstari wa mbele) akiwa na viongozi wengine na watumishi wa Mahakama ya wilaya Rorya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki akisaini kitabu cha wageni katika Mahakama ya Wilaya Serengeti.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati mstari wa mbele) akiwa pamoja na Naibu Msajili, Mhe. Omari Kingwele (wa kwanza kushoto), Mtendaji wa Mahakama, Bw. Leonard Maufi (wa kwanza kulia), Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Tarime, Mhe. Stanley Mwakihaba (wa pili kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mtana-Tarime, Mhe. Godfrey Muroba (wa pili kushoto) pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Wilaya Tarime na Mtana.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati) akiwa na viongozi wengine baada ya ukaguzi wa Gereza la Wilaya Tarime.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Mahakama na wadau wa Mahakama baada ya ukaguzi wa Gereza la Mahabusu na Wafungwa Mugumu-Serengeti.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omari Kingwele akifafanua jambo wakati wa ukaguzi.

Mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, Bi. Berther Lucas (aliyesimama) akitoa maoni, huku watumishi wengine wakifuatilia, wakati wa kikao cha ukaguzi.

Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bunda wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati mstari wa mbele) baada ya ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki baada ya ukaguzi wa Mahakama hiyo. Wengine katika mstari wa mbele ni Naibu Msajili, Mhe. Omari Kingwele (wa pili kulia), Mtendaji wa Mahakama, Bw. Leornard Maufi (wa kwanza kulia), Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Mhe. Theotimus Swai (wa pili kushoto) na Afisa Rasilimali Watu, Bi. Francisca Swai (wa kwanza kushoto).

Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Musoma, Mahakama za Mwanzo Musoma Mjini na Mukendo wakimsikiliza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (hayupo pichani).

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Jamaica.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni