Na ARAPHA RUSHEKE – Mahakama, Dodoma
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, imefanya vikao mbalimbali na wadau wa
utoaji haki kwa lengo la kujadili hali ya mashauri, changamoto zinazojitokeza
katika uendeshaji na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji haki kwa wakati.
Vikao
hivyo vilivyofanyika tarehe 18 Septemba, 2026 katika ukumbi wa Mkutano kwenye
Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki vilijumuisha Kikao cha Bench-Bar, Kikao cha Madalali wa Mahakama pamoja na Wasambazaji
wa Nyaraka za Mahakama, na viliongozwa na Jaji Mfawidhi, Mhe. Joachim
Tiganga.
Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe Upendo Ngitiri, aliwasilisha hali ya mashauri ya
madai na ukazaji hukumu, ikiwemo mashauri yaliyobaki, mashauri ya mlundikano na
hatua zinazochukuliwa na Mahakama katika kuhakikisha mashauri yanashughulikiwa
na kukamilishwa kwa wakati.
Vikao
hivyo pia vilijadili changamoto mbalimbali zinazoweza kusababisha ucheleweshaji
wa mashauri, huku wadau wakishirikishana uzoefu na kutoa mapendekezo ya namna
ya kukabiliana na changamoto hizo.
Miongoni
mwa mikakati iliyosisitizwa ni kuendelea kufanya vikao maalum vya kusafisha
mashauri, kupunguza ahirisho zisizo za lazima, kupanga mashauri kwa kuzingatia
utayari wake, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Mahakam ana wadau.
Vilevile,
Mahakama imeendelea kuhimiza matumizi ya njia zinazosaidia kuharakisha
usikilizaji wa mashauri, ikiwemo matumizi ya taarifa za mashahidi na
mawasilisho kwa njia ya maandishi pale inapofaa.
Akifunga vikao hivyo, Mhe. Tiganga alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwajibikaji wa kila mdau katika kuhakikisha mashauri yanashughulikiwa kwa ufanisi na wananchi wanapata haki kwa wakati.
Meza
Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe.
Joachim Tiganga (aliyeka katikati). Kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama
Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri na kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama Dodoma.
Meza
Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe.
Joachim Tiganga (aliyeka katikati)ikiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
waliohudhuria kikao hicho .
Wajumbe
walioudhuria wakifuatilia kwa makini kikao hicho.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Joachim Tiganga (wa kwanza
kulia) akieleza jambo wakati wa kikao hicho. Kushoto kwake ni Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri.
Meza
Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe.
Joachim Tiganga (aliyeka katikati). Kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama
Kuu Dodoma, Mhe. Upendo Ngitiri na kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mahakama ya
Hakimu Mkazi Dodoma, Mhe. Thurston Kombe, wakiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe waliohudhuria kikao hicho.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Jamaica.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni