Jumatano, 2 Septemba 2026

JAJI MFAWIDHI MUSOMA AMUAPISHA AFISA USULUHISHI

Na FRANCISCA SWAI – Mahakama, Musoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki, tarehe 31 Agosti, 2026 alimwapisha Bw. Said Mmbando, kuwa Afisa Usuluhishi II.

Uapisho huo ulifanyika ofisini kwa Jaji Mfawidhi na kushuhudiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora, Mtendaji wa Mahakama Musoma, Bw. Leonard Maufi, pamoja na Msuluhishi Mkuu II, Bw. Peter Mahindi.

Pamoja na uapisho huo, Mhe. Kakolaki alitoa nasaha kwa Bw. Mmbando kufanya kazi hiyo bila upendeleo, huba au chuki. Alimsihi siku zote atambue kuwa kazi ya uamuzi ni kazi ya Mungu, hivyo aifanye kwa uadilifu na weledi mkubwa kwa zingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo.

Uapisho wa Afisa Usuluhishi II, Bw. Said Mmbando (kulia), mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (aliyesimama katikati), ukishuhudiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora, Mtendaji wa Mahakama Musoma, Bw, Leonard Maufi, pamoja na Msuluhishi Mkuu II, Bw. Peter Mahindi.

Afisa Usuluhishi II, Bw. Said Mmbando (kulia) akisaini kiapo chake mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto).

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto), akisaini kiapo cha Afisa Usuluhishi II, Bw. Said Mmbando (katikati) wakati Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (kulia) akishuhudia tukio hilo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto), akimkabidhi hati ya kiapo Afisa Usuluhishi II, Bw. Said Mmbando (katikati) wakati Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (wa pili kulia) pamoja na Msuluhishi Mkuu, Bw. Peter Mahindi (wa kwanza kulia) wakishuhudia tukio hilo.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Morogoro.

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni