Jumanne, 1 Septemba 2026

JAJI MWENDA ANGOZA ZOEZI LA USAFI SINGIDA

Na EVA LESHANGE & AMIRI BAKARI, Mahakama Singida

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Singida, Mhe. Ayoub Mwenda tarehe 29 Agosti, 2026 aliwaongoza watumishi katika zoezi la usafi ikiwa ni jitihada za kuhakikisha mazingira yanakuwa safi licha ya kuwa na watoa huduma ya usafi sambamba na kujenga utamaduni wa kutunza mazingira na kujenga mahusiano mazuri baina ya watumishi na kuimarisha umoja.

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu Singida aliwaeleza kuwa, zoezi hilo ni endelevu na litakuwa likifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi likihusisha hadi Mahakama za ngazi za chini.  

“Watumishi wenzangu kufanya usafi ni mojawapo ya mazoezi ya viungo lakini pia ni utaratibu mzuri kwani unaimarisha umoja na mshikamano mahala pa kazi na pia kila mmoja wetu atakuwa balozi katika masuala ya utunzwaji wa mazingira kama tulivyoona usafi sio jambo rahisi na zoezi litakuwa endelevu na litahusisha Mahakama ngazi za chini,” alisema Mhe. Mwenda.

Mahakama zilizofanya usafi kwa siku hiyo ni pamoja na Mahakama ya Wilaya Singida, Mahakama ya Wilaya Manyoni, Mahakama ya Mwanzo Itigi, Mahakama ya Mwanzo Mgandu, Mahakama ya Mwanzo Ikungi, Mahakama ya Mwanzo Ipembe na Mahakama ya Mwanzo Utemini.

Aidha, watumishi wamefurahishwa na zoezi hilo ambalo limeleta tija kwa kuonesha jukumu la usafi ni la wote hivyo, wameahidi kuwa mabalozi wazuri katika utunzaji wa Mazingira.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Singida, Mhe. Ayoub Mwenda akiwaongoza Watumishi wa Mahakama hiyo kufanya usafi tarehe 29 Agosti, 2026.

  
   Watumishi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Singida wakiwa katika usafi wa Pamoja uliofanyika katika jengo la Mahakama Kuu tarehe 29 Agosti,2026.


 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Singida, Mhe. Fadhili Luvinga akifanya usafi.

Msaidizi wa Kumbukumbu  Mahakama ya Mwanzo Ikungi, 
Bi. Magreth Mtilimbania akiwa katika zoezi la usafi.

  Mhe. Aggrey Muhigi wa Mahakama ya Mwanzo Mgandu akifanya usafi.

  Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni kwa wakiendelea kufanya usafi kwa pamoja.


Msaidizi wa Kumbukumbu Mahakama ya Mwanzo Itigi, Bi.Mwajuma Sudi akiwa katika zoezi la kufanya usafi.

  Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Utemini Singida wakiendelea na zoezi la kufanya usafi kwa pamoja.


  Watumishi wa Mahakama Kuu Singida wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha zoezi la usafi. Aliyesimama mstari wa kwanza wa tatu kulia ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Singida, Mhe. Ayoub Mwenda, kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Singida, Mhe. Fadhili Luvinga, wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Singida, Bw. Filbert Matotay, wa kwanza kulia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Singida, Mhe. Aloyce Masua na wa pili kushoto ni Msaidizi wa Sheria wa Jaji, Mhe. Mariam Hamisi.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni