Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Dodoma.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, jana tarehe 5
Octoba, 2026 alikutana na kuzungumza na watumishi wapya wa kada ya ulinzi waliopangiwa
kufanya kazi katika Mkoa wa Dodoma.
Mazungumzo
hayo yalifanyika katika ukumbi wa mkutano kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki
Dodoma na kuhudhuriwa na Mtendaji wa Mahakama Dodoma, Bw. Bedson Mariba, pamoja na Wakuu wa Vitengo mbalimbali wa
Mahakama hiyo.
Katika mazungumzo hayo, Jaji Mfawidhi aliwakaribisha watumishi hao na kusisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi na uwajibikaji. Mhe. Tiganga aliwahimiza watumishi hao kuzingatia misingi ya utumishi wa umma na kulinda heshima ya Mahakama.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim
Tiganga, akisikiliza utambulisho kutoka kwa watumishi wapya (hawapo katika picha).
Mtendaji
wa Mahakama Dodoma, Bw. Bedson Mariba, akielekeza jambo wakati wa
kuwatambulisha watumishi wa ajira mpya (hawapopichani).
Meza
Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo
Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na watumishi ajira mpya. Kushoto kwake ni Mtendaji wa Mahakama Dodoma, Bw. Bedson
Mariba na kulia kwake ni Mlinzi Mwandamizi wa Mahakama Kuu Dodoma, Bi Naima
Mandai.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma pamoja na watumishi ajira mpya
wakimsikiliza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma,
Mhe. Joachim Tiganga (hayupo kwenye picha) alipokuwa nazungumza na watumishi
hao.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni